Habari za Punde

Breaking News... Mwakilishi wa Jimbo la Bububu Afariki Asubuhi Hii

Mwakilishi wa Jimbo la Bububu wa  Chama cha Mapinduzi Salum Ali Mtondoo, amefari dunia leo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja akiwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi ICU,

Taarifa iliotolewa na Spika wa Baraza la Wawakilishi  wakati akifunguwa Mkutano wa Uvuvi katika hoteli ya Zanzibar Beach, na kutoa taarifa hiyo.

Amewataka Wanafamilia na Jamaa zake kuwa na moyo wa Subira kwa pendo la ndugu yao huyo mpenda kwa kuwa kuondoka kwake ni pengo lakini muda umeshafika hakuwa na kulizui.Pia amesema Mhe Salum ameacha pengo katika Baraza la Wawakilishi na kwa Wananchi wa Jimbo lake la Bububu, amewataka kuwa na Subra.

Amesema Taratibu zote za mazishi zinatayarishwa, aytapelekwa katika ukumbi wa bara kwa kuuaga mwili wa marehemu na kuusomea dua kabla ya kuupeleka kijiji kwao Bumbwini kwa mazishi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.