Habari za Punde

Maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani 23 March



Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Zanzibar Hamad Masoud, akiwahutubia Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Kanda ya Zanzibar na Wanafunzi katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani huadhimishwa kila mwaka 23 March.  
Mkurugenzi wa Kanda Khamis Ali Suleiman, akitowa historia ya siku ya Hali ya Hewa Duniani katika sherehe za maadhimishom hayo yaliofanyika katika viwanja vya Ndege Kiembesamaki Zanzibar.  
Wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Zanzibar, ambao hutoa huduma wakiwa katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani.

Wanafunzi wa Skuli ya High View wakimsikiliza Waziri wa Mawasiliano na akihutubia katika sherehe hiyo, wakiwa makini nkumsikiliza  akitowa nasaha zake kwa Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Zanzibar.  
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Zanzibar wakiwa katika sherehe hizo.
Wanafunzi wa Skuli ya Kiembesamaki wakihudhuria sherehe hizo za  Maadhimisho ya Hali ya Hewa Duniani yakiadghimishwa katika Viwanja vya Ndege vya Zanzibar.
Mfanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Zanzibar, akitowa maelezo kwa Wanafunzi wa Skuli waliotembelea kuona utendaji wa uchunguzi wa hali ya hewa na utabiri wa hali ya hewa vinavyotumika katika kazzi zao za utabiri, wanafunzi hao wamepata fursa za kuuliza maswali mbalimbali yanayotokana na utabiri.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.