Habari za Punde

NEC Isiwafumbie Macho Wapinzani Matusi

Na Mustafa Leu, ARUSHA

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imeshauriwa kutovifumbia macho vyama vya siasa vinavyoshabikia vurugu kwenye kampeni zinazoendelea za uchaguzo mdogo jimbo la Arumeru Mashariki.

Mjumbe wa halmashauri Kuu ya CCM, Christopher Ole Sendeka, alieleza hayo kwenye mkutano wa kampeni za katika kata ya Nkoanrua, alipokuwa akimnadai mgombea wa chama hicho Sioi Sumari.

Sendeka alisema NEC inatakiwa kutovionea haya vyama vyenye kushabikia vurugu na badala yake vichukuliwe hatua kama vimeshindwa kufanya kampeni za kistaarabu.
Alisema Tume haitakiwi ikae kimya huku baadhi ya viongozi wakuu na wafuasi wa vyama vya upinzani wakiwatukana viongozi wa kitaifa kwenye kampeni za uchaguzi.

Alisema ni kitendo cha fedha na aibu kwa viongozi wa upinzani kuwashambulia kwa lugha kali viongozi wastaafu wa kitaifa wakiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa na waziri Mkuu mstaafu Edward Lowasa.

Sendeka alisema kuwashambulia viongozi hao wenye heshima kubwa ndani na nje ya taifa ni kinyume na maadili ya uchaguzi na ni vitendo visivyokubalika.

Alisema umefika wakati vyama vya siasa kutambua kuwa vinatakiwa viwaeleze wananchi nini watakachokifanya endapo watapewa ridhaa na sio kutumia majukwaa kuwatukana viongozi wa kitaifa ambao wamelifanyia mambo mengi taifa.

Kwa upande wake mratibu wa kampeni za uchaguzi, Lameck Mwigulu, aliwakumbusha wananchi kuwa katika uchaguzi huo hautabadilisha serikali bali ni kuziba pengo.

Alisema ni kweli katika jimbo hilo kuna matatizo lakini mwenye majawabu ya kuyatatua ni serikali ya Chama cha Mapinduzi iliyoko madarakani, na si chama kingine ambacho hakina serikali.

“Duniani kote serikali ikishaingia madarakani sera na mipango inayotekelkezwa ni ya serikali iliyopo madarakani hivyo wananchi msisipandikizwe hasira nanyi mkakafanya maamuzi ya hasira kwa kuuchagua upinzani”, alisema.

Aliongeza kuwa hata wapinzani wanaopita pita na kudai kuwa miaka 50 ya Uhuru hakuna lililoofanyika wanatambua kuwa mipango inayotekelezwa ni ya serikali ya Chama cha Mapinduzi, hivyo wapuuzeni kwa kuwanyima kura.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.