Habari za Punde

Serikali Itaongeza Nguvu Sekta ya Uzalishaji Kupitia Vikundi vya Ushirika - Balozi Seif

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akizungmza na Viongozi wa CCM WA Mkoa wa Kaskazini Pemba Kwenye Ukumbi wa Skuli ya Micheweni Pemba.
Kushoto yake ni Mwenyekiti wa CC Mkoa wa Kaskazini Pemba Nd. Mberwa Hamad Mberwa, kulia yake ni Mjumbe wa Kamatiya Siasa ya Mkoa huo Mh. Dadi Faki Dadi na Pembeni yake ni Mke wa Balozi Seif Mama Asha Suleiman Iddi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kikagua Maendeleo ya Ujenzi wa Tuta la kuzuia Maji ya Bahari yasivamie mashamba ya Kilimo cha Mpunga katika Bonde la Mziwanda Wilaya ya Micheweni
Katibu wa Ushirika wa Ufugaji Samaki wa Kishakaashishangi wa Kiuyu Minungwini Nd. Othman Bakari akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ai Iddi jinsi ya harakati za Mradi wao ulioanzishwa mwaka 1994.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifurahia kazi za mikono zinazoendeshwa na Kikundi cha Ushirika cha Tuvumiliane Women Group kiliopo Mjini Wete akiwa pamoja na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi. Balozi Seif alihamasika kuchangia shilingi 500,000/- wakati Mama Asha akachangia shilingi 300,000/- kuuendeleza Ushirika huo.


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imelenga kuongeza nguvu zaidi katika Sekta ya Uzalishaji kupitia Vikundi vya uzalishaji mali ili kuwajengea mazingira mazuri Wananchi katika kujiwezesha Kiuchumi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema hayo akiwa katika ziara ya siku tatu Kisiwani Pemba kukagua Miradi ya Maendeleo baada ya kuvitembelea vikundi vya Ushirika vya Tuvumiliane Women Group Wete, ushirika wa Ufugaji Samaki na Mradi wa Chumvi Kiuyu Minungwini.

Pia alikagua tuta litakalozuia maji ya bahari ili kunusuru Eka 61 za Kilimo cha Mpunga zinazolimwa na wakulima wa Mpunga wa Bonde la Mziwanda Wilaya Micheweni.


Balozi Seif akizungumza katika mikutano tofauti ndani ya ziara hiyo alisema suala la Vikundi vya Ushirika 
limetiliwa mkazo ndani ya Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 ya kulenga kuviimarisha vikundi vya Ushirika.

Alisema kumekuwa na mafanikio makubwa kwa jamii na Wananchi ambao wameamua kuunda Vikundi vya Ushirika jamnbao ambalo limekuwa likileta faraja.

Balozi Seif amevipongeza vikundi hivyo kwa kukubali kwao kuitikia wito wa Serikali wa kujiajiri wenyewe na hatimae kujiongezea mapato yanayowawezesha kujikimu kimaisha pamoja na kuhudumia familia zao Kielimu.

“ Nia ni ile ile ya kuundwa Vikundi vya Ushirika ili kujiendeleza Mairdi yao ya Uzalishaji Mali”.Alisisitiza Balozi Seif.

Alivitaka Vikundi hivyo kujiendeleza zaidi kwa kudumisha uaminifu na uadilifu miongoni mwao hali ambayo itavifanya vikundi hivyo viendelee kudumu zaidi kiuzalishaji.

“ Mkianza kutiliana Mashaka kwa dhana ya Mwenyekiti au Mhasibu kula kula fedha za Wanaushirika hamtafika popote pale” Alitahadharisha Balozi Seif Ali Iddi.

Alisisitiza kwamba Serikali kupitia Taasisi na Mashirika hisani yatajaribu kuangalia njia zitakazosaidia kuvipa msukumo Vikundi hivyo kwa nia ya kuvijengea uwezo ulio bora.

Katika Risala zao Vikundi hivyo vimeelezea changamoto zinazowakabali wana Vikundi hao ikiwa ni pamoja Vifaa vya kufanyia kazi,Utaalamu pamoja na ukosefu wa mashine ya kukaushia kwa kikundi cha ushirika cha Tuvumiliane Women Group.

Mapema Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar Dr. Kassim Gharib alisema ongezeko la Miradi ya ufugaji Samaki limeongezeka na kufikia Miradi 125 Unguja na Pemba.

Dr Gharib alisem a hali imekuja kufutai utafiti uliofanywa na Wataalamu na kubaini kwamba maeneo ya Ufugaji Samaki ndani ya Visiwa vya Zanzibar Kimazingira ni mazuri.

KatibuMkuu huyo wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi alifahamisha kwamba katika kuipa nguvu Sekta ya Ufugaji Samaki Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China imekubali kusaidia kutoa Taaaluma katika Sekta hiyo.

Alisema Taaluma hiyo itahusisha kuwajenhgea uwezo zaidi Wataalamu wa Wizara hiyo pamoja na kuwapatia mafunzo ya moja kwa moja Wafugaji wenewe kuligana na taratibu zitakavyopangwa.

Katika ziara hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alichangia Shilingi 500,000/- kwa ajili ya kukiendeleza Kikundi cha Ushirika cha Tuvumiliane Women Group cha Wete wakati Mke wa 

Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman Iddi akakichangia Kikundi hicho Shilingi 300,000/-.
Mama Asha pia akasaidia nguvu kazi ya shilingi 200,000/- kwa akina mama wanaojitolea katika ujenzi wa Daraja kwenye tuta la Bonde la Mziwanda Micheweni ambao wao ndio wanaoonekana kuathirika zaidi kutokana na mashamba yao ya Mpunga kuvamiwa na maji ya Chumvi.


Othman Khamis Ame Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.