Habari za Punde

Serikali Yaombwa Kukisaidia Walimu Kituo cha Soba House Kijichi

Zalha Kassim-MCC 07/03/2012

Serikali imeombwa kukipatia kituo cha Soba House cha Kijichi Walimu wenye uzoefu ambao wataweza kuwasaidia vijana wa kituo hicho kuweza kubadili vyema tabia zao ili waweze kuanzisha maisha mapya yenye malengo.

Ombi hilo limetolewa na msimamizi wa kituo hicho, Valantia Muhammedi Ali alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi Afisini kwake kuhusiana na maendeleo ya kituo chake.


Amesema kwa sasa wanajiongoza wenyewe katika kituo hicho bila kuwa na mtaalamu yeyote wa Ushauri nasaha ambae anaweza kutoa muongozo mzuri wenye kueleweka.

Muhammed amesema kukosekana kwa Walimu katika kituo chao kumepelekea baadhi ya vijana waliopo katika kituo hicho kukosa kuyatilia maanani maelekezo na nasaha ambazo zimekuwa zikitolewa na wakubwa wao kwa madai kuwa ni ya wao kwa wao.

Amesema ana uhakika kwamba ikiwa kutaletwa mtaalamu ni wazi kuwa mabadiliko yatapatikana na vijana kuongezeka ari ya kuendelea kuwa mabalozi wema kwa wengine ambao bado wanaendelea kutumia madawa ya kulevya katika maisha yao.

Ameongeza kuwa vijana watakapo achana na madawa ya kulevya ni wazi taifa letu litakua na vijana bora wenye nguvu na ari katika kujenga na kutetea maslahi ya Taifa

Akielezea mafanikio ambayo wameyapata kituoni hapo tokea kuanzishwa kwake amesema ni pamoja na kuweza kuwatoa vijana katika majanga maovu ya ulevi na kuwaweka pamoja ambapo hali za afya zao zinaendelea vizuri

Kwa upande wa changamoto ambazo wanakabiliana nazo kituoni hapo ni pamoja na migongano ya mara kwa mara miongoni mwa vijana,kutoroka na kukosa kulipa ada katika muda muafaka

Aidha Muhammed amesema wapo katika mchakato wa kutafuta Wafadhili ili wapate kuwasaidia katika shuhuli zao mbalimbali zinazowakabili katika kituo hicho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.