Akizungumza katika uzinduzi wa kanuni ya msumeno wa moto katika afisi za wizara hiyo maruhubi amesema matumizi ya msumeno wa moto yanasabisha uharibifu mkubwa wa rasilimali ya misitu na kusababisha wasiwasi kutoweka kabisa na kuifanya nchi kukumbwa na hali ya ukame.
Ametaka uzinduzi wa kanuni hizo uchochee usimamizi mzuri wa misitu kwa lengo la kunusuru kukatwa kwa miti ya matunda, misitu na miti ya biashara ili isitoweke.
Mhe Ramadhani Abdalla Shaaban amesema serikali kupitia wizara ya kilimo na mali asili itaendelea kuhamasisha jamii kujenga tabia ya upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali nchini.
Wakati huo huo Mhe Ramadhani Abdalla Shaaban amekabidhi vifaa vya maabara ya mifugo kwa wizara ya mifugo na uvuvi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi millioni mia moja hamsini na moja.
Ametaka vifaa hivyo vitumike kama ilivyokusudiwa kwa mujibu wa mipango kazi na matumizi yake yafuate taratibu na kanuni za serikali.
Ameushukuru mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo ifad kwa kuwapatia mkopo unaowezesha kutekeleza shughuli mbalimbali za kuinua hali za maisha ya wakulima na wafugaji nchini.
Chanzo cha Habari ZBC Redio.
No comments:
Post a Comment