Na Ali Muombwa ZBC
Kamishna wa Elimu Zanzibar Bi Mariam Abdalla amesema kuna umuhimu kwa Zanzibar kushirikiana na Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki katika kuimarisha huduma za Elimu Mjumuisho maskulini.
Akifunga mkutano wa siku nne uliowajumusha Wahadhiri wa Vyuo na Taasisi zinazohusika na utoaji wa Elimu Mjumuisho kutoka Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki huko katika Ukumbi wa Ggrand Palace Hotel Malindi amesema ingawa Zanzibar imepiga hatua lakini bado inahitaji mbinu za ziada zilizo za kitaalamu zaidi ili iweze kupata mafanikio ya Kimataifa.
Amewashauri Wajumbe wa Mkutano huo kufikiria utaratibu wa kuwa na Mitaala na mbinu za pamoja ili kufikia malengo sawa katika kuwapatia haki ya elimu watoto wenye ulemavu.
Nae Mkuu wa Chuo cha Kiislamu Zanzibar Dk Muhidin Ahmad amesema hatua ya Chuo hicho kuanzisha Mafunzo ya Elimu Mjumusho ni miongoni mwa mikakati ya Zanzibar ya Elimu kwa wote iliyomo ndani ya sera ya Elimu Zanzibar.
Amesema Mkutano huo wa Kumi na Tatu ni wa mwanzo kufanyika Zanzibar chini ya Uenyeji wa Chuo cha Kiislamu Zanzibar na umeleta changamoto kubwa na kuahidi kuyafanyia kazi maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano huo.
nMUNGANO UVUNJIKE TENA WASAIDIENI WALEMAVU
ReplyDelete