Habari za Punde

Jaji Mkuu wa Zanzibar Atatoa Adhabu kwa Watendaji wa Mahakama.

Na Mwandishi Shomari. 

Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu amesema atahakikisha anatoa adhabu kali kwa watendaji wote wa Mahakama ikiwa ni pamoja na Mahakimu watakaogundulika na vitendo vya kupokea rushwa.

Akizungumza kwa nyakati tafauti wakati alipokuwa katika ziara ya kujitambulisha kwa Wanafunzi wafungwa na walioko rumande katika Magereza ya Kiinua Miguu Kilimani, Langoni na Kinumoshi amesema atahakikisha anachukua jitihada za makusudi kukabiliana na vitendo vyote vya rushwa dhidi ya Watendaji wa Idara ya mahakama ili kuhakikisha haki inapatikana kwa kila mwananchi.

Amesema atahakikisha Kesi na Rufaa zote zilizowasilishwa na wanafunzi (wafungwa) wote na rumande zinasikilizwa kwa wakati ili haki itendeke na kupunguza mlundikano wa wanafunzi wafungwa na rumande gerezani.

Jaji Makungu amesisitiza kuwa atawaomba Wajumbe wa Baraza la Wawakilisha kuongeza Bajeti kwa Chuo cha Mafunzo ili kuweza kumudu mahitaji muhimu ikiwemo chakula na dawa kwa wale walioko kizuizini.

Mapema Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Khalifa Hassan Chum amewataka wanafunzi wafungwa na rumande kutoa maombi na malalamiko yao bila woga.

Katika risala yao wanafunzi wafungwa pamoja na rumande wamemuomba Jaji Makungu kuwaelimisha Mahakimu kutoa masharti mepesi watayoyaweza ili waweze kuepukana na kukaa rumande kwa muda mrefu.

Ziara hiyo itaendelee kesho kwa kutembelee kambi za Ubago na Hanyengwa mchana.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.