Habari za Punde

Idara ya Uvuvi na Mazao ya Baharini yateketeza zenye thamani ya shilingi milioni 30

 Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi na Mazao ya Baharini Mussa Aboud Jumbe, akionesha picha inoyoelezea jinsi samaki anavyoaza kikua hadi kufikia kufuliwa kama wavuvi watatumia nyavu zinazostahili kuvulia, ambazo zitawaacha samaki wadogo na kuwavua wakubwa na wadogo kuendelea na kukuwa.  
 Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi na Mazao ya Baharini Mussa Aboud Jumbe, akiwaonesha  kitabu chenye  tafiti za Wavuvi  na jinsi ya uvuvi wanaotumia na kuonesha hesabu ya Wavuvi wanaofanya kazi hiyo kutokana na sensa ya mwaka 2010 inaonesha wavuvi walioko Zanzibar ni 34,000.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uvuvi Mussa Aboud Jumbe akitowa maelezo jinsi ya kupiga vita uvuvi harama wa kutumia Nyavu zisizostahili, ambazo hugharibu mazalio ya samaki na kuvua samaki bado ni wadogo  hawastahili kuvuliwa. 
 Makatibu wa Kamati za Vijiji za Uvuvi Zanzibar wakionesha moja ya nyavu zilizokamatwa hutumika katika uvuvi usiostahili.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi na Mazao ya Baharini Mussa Aboud Jumbe, akiwaonesha waandishi wa habari moja ya Nyavu iliosalimishwa na Mvuvi  mwenyewe ambayo ina thamani ya shilingi milioni 17, wamefanya maungumzo nae kumpatia nyenzo za kufanyika kazi. kuepuka matumizi ya kutumia vyavu haramu. 
 Mkuu wa Doria wa Idara ya Uvuvi na Mazao ya Baharini Haji Shomari, akiwaonesha waandishi wa habari moja ya nyuvu nzito walizozikamata zikitumika katika uvuvi, ambayo hujulikana kwa jina la Mfuko .

 Uvuvi wa kutumia mikuki umepigwa marufuku kwa ajili ya matumizi yake huharibu matumbawe na mazalio ya samaki baharini, ikipelekwa kuangamizwa.
 Vijana wakikusanya Nyavu zilizokamatwa zenye macho madogo, kwa ajili ya kuzitelekeza. 
 Makatibu wa Kamati za Uvuvi za Vijiji wakishusha nyavu katika gari ili kwa ajili ya kuziangamiza.
 Makatibu wa Kamati za Uvuvi katika Madiko mbalimbali ya Zanzibar wakishudhudia zoezi hilo linafanyika la kiziteleteza  Nyavu zilizokamatwa kutokana na kutumika kinyume cha sheria ya Uvuvi ya Zanzibar. inayopiga marufuku utumiaji wa nyuvu zenye macho madogo huvua samaki wasiostahili.
 Nyavu zilizokamatwa ambazo zimepigwa marufuku kutumika katika uvuvi kutokana na  sheria ya uvuvi inayotumika Zanzibar, zikiteketea kwa moto katika zoezi hilo lililofanyika katika viwanja vya Idara ya Uvuvi Kinazini. ambazo zimekamatwa.
 Mkuu wa Doria wa Idara ya Uvuvi na Mazao ya Baharini Haji Shomar, akitowa  maelezo kwa Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kusini Makunduchi Khamis Rashid Khamis, akishuhudia zoezi hilo linavyoendelea  ili kuhakikisha  nyavu hizo zinatiwa moto kwa mujibu wa sheria ya Uvuvi.  
 Makatibu wa Kamati za Uvuvi za Vijiji wakibadilishana mawazo jinsi ya kazi zao wanazofanya kuhakikisha utumiaji wa uvuvi haramu na vifaa vilivyopingwa marufuku kutumika katika uvuvi,kutoka kulia Haji Mati, (Tazari)Khamis Ali Hamdu (Kigunda) na Haji Khamis Haji (Kendwa) wakiwa katika viwanja vya zoezi la uchomaji wa nyavu hizo Ofisi ya Idara ya Uvuvi Kinazini.
Katibu wa Kamati ya Uvuvi ya  Ghuba ya Minai Suleiman Mohammed, akizungumza na waandishi wa habari katika zoezi la kuangamiza Nyavu  zenye macho madogo aqmbazo haziruhusiwe kutumika katika Uvuvi , jinsi ya changamoto wanazotowa kwa Idara ya  Uvuvi  kupambana na baadhi ya Wavuvi ambao bado hutumia  mitengo hivyo  inayoharibu mazingira na kuvua samaki wadogo.   

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.