Watu 46,000 waathiriwa na mafuriko Comoro
MORONI,Comoro
OFISI ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia majanga kimaumbile (OCHA) imesema, watu zaidi ya 46,000 visiwani Comoro wameathiriwa na wengine 9,000 wamepoteza makazi yao kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyoanza kunyesha kuanzia Aprili 20.
Tathmini ya awali iliyofanywa na serikali ikishirikiana na Umoja wa Mataifa na Shirika la hilali nyekundu visiwani humo, inaonesha kwamba misaada ya maji safi, dawa, chakula, makazi, elimu na mawasiliano inahitajika.
Serikali ya Comoro imetangaza hali ya hatari nchini humo.
Ofisi hiyo ya Umoja wa Mataifa imeonya kuwa mvua zinazoendelea kunyesha zitasababisha watu zaidi kupoteza makazi yao na kuwa na mahitaji zaidi ya misaada.
Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ikiwemo OCHA, na lile linalowahudumia watoto UNICEF pamoja na Shirika la Mpango wa Chakula WFP yanatuma misaada ya kibinadamu visiwani humo. (Reuters).
Maskini ndungu zetu!
ReplyDeleteMungu awasaidie na awape moyo wa subra na kuamini kwamba hayo yote yanatoka kwake!
Sisi wengine kutokana na uwezo wetu mdogo tutashindwa kuwasaidia moja kwa moja labda viongozi wetu wa miskiti waamue kuchangisha ndio misaada ya akina sisi itawafikia vinginevyo tutaishia DUAA!