Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar,waliofika Ikulu Mjini
Zanzibar leo.[Picha na Ramadhan Othman.Ikulu.]
Na Idara ya H/Maelezo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dk Ali Mohammed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani May Day huko Bwawani Mjini Zanzibar
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa naWizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kupitia kamisheni ya kazi imeeleza kwamba Sherehe hizo zitaanza saa mbili asubuhi kwa maandamano maalum ya Wafanyakazi kutoka Taasisi mbali mbali za sekta za Ummma na Binafsi.
Baada ya mapokezi hayo Rais wa Zanzibar anatarajiwa kuzungumza na Wafanyakazi wa Zaznibar na baadae kukabidhi zawadi kwa wafanyakazi bora kutoka tasisi mbali mbali.
Mapema Mwakilishi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) atatoa salam zake kwa wafanyakazi wa Zanzibar ikifuatiwa na risala ya wafanyakazi..
Mapema waandaaji wa wamaadhimisho hayo ya Siku ya Wafanyaklazi Duniani (MEI DAY) ambao ni Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ikishirikiana na Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi (ZATUC) watafanya usafi wa mazingira kuanzia tarehe 27 hadi 30 mwezi huu katika maeneo ya Hospitali ya Mnazi Mmoja.,Nyumba za Wazee Sebleni ,Hospitali ya Wagonjwa wa Akili na Afisi za ZATUC Kikwajuni.kuanzia saa 1.00 asubuhi kwa siku zote hizo.
Aidha taarifa hiyo imeviomba vyombo vya Habari kutoa ushrikiano wao katika kushiriki kikamilifu kwenya Sherehe hizo na kuwapa taarifa wanahi wa Tanzania juu ya siku hiyo muhimu.
Siku ya Wafanya kazi Duniani hufanyika kila tarehe 1 Mei Ulimwenguni kote
No comments:
Post a Comment