Baadhi ya Masheikh waliohudhuria katika Mkutano wa Waziri wa Katiba na Sheria Abubakari Khamis Bakari wakisikiliza kwa makini maelezo mbalimbali yaliokuwa yakitolewa kuhusiana na mchakato wa Katiba mpya na mihadhara inayofanywa sehemu mbalimbali za Zanzibar.
Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Abubakar khamis Bakari akifafanua jambo katika mkutano na Baadhi ya Masheikh wa jumuia mbalimbali za kiislam kuhusiana na mchakato wa Katiba mpya na mihadhara inayofanywa sehemu mbalimbali za Zanzibar.Kulia yake ni Waziri wa nchi afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohd Aboud na kushoto yake ni Kadhi Mkuu wa Zanzibar sheikh khamis Haji.
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohd Aboud akifafanua jambo katika mkutano na Baadhi ya Masheikh wa jumuia mbalimbali za kiislam kuhusiana na mchakato wa Katiba mpya na mihadhara inayofanywa sehemu mbalimbali za Zanzibar.Kulia yake ni Waziri katiba na Sheria wa Zanzibar Abubakar Khamis na kushota yake ni WAziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Mwinyihaji Makame.
Amiri kutoka katika Jumuiya ya Uamsho Mselem Ali akielezea jambo katika mkutano na Waziri wa Katiba na Sheria Abubakari Khamis kuhusiana na mchakato wa Katiba mpya na mihadhara inayofanywa sehemu mbalimbali za Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu CUF Ismail Jusa Ladhu akifafanua jambo katika mkutano na Waziri wa Katiba na Sheria Abubakari Khamis kuhusiana na mchakato wa Katiba mpya na mihadhara inayofanywa sehemu mbalimbali za Zanzibar kulia yake ni Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai.
Hawa jamaa, tunawapenda kama viongozi wetu wa dini lkn. wanatusikitisha kutokana misimamo yao iliyokosa upeo wa siasa za kimataifa.
ReplyDeleteLeo hii, nchi yeyote duniani inayotafuta mabadiliko hata kama ni ya haki kwa kutumia vikundi vya dini ya kiislamu, nchi za magharibi zinahakikisha hazifanikiwi.
Sielewi kwanini wasomi wachache wa Z'bar waliopatikana kutokana na miaka 40 ya elimu bila malipo( kuazia primary to University level) wakaamua kutumia vikundi vya kiislamu badala ya Wabunge wetu?
Tunatakiwa tuangalie mifano ya ndugu zetu TWALIBAN walivyoondolewa madarakani, HAMAS walivyoekewa vikwazo TUWAREG wanaodai taifa la AL- ZAWAD huko Mali wanavyoundiwa zengwe na Ufaransa, na wote hawa wana madai ya haki.
Huko nyuma, hofu ya siasa kali za kiislamu ilikua moja ya sababu zilizotumiwa kuiingiza Z'bar kwenye muungano na leo watu wanafanya yale yale!..yako wapi matunda ya elimu bila malipo?
Misimamo ya kipumbavu hii, imewadhuru ndugu zetu SUDAN INGAWA KESI YAO NI TIFAUTI KIDOGO NA YETU lkn. wahafidhina kule walipinga wakristo kupewa haki ktk nchi, matokeo yake kusini wamejitenga na kuchukua utajiri kariba wote wa iliyokua sudan.
Kilichotokea Sudan sasa wanafanya vitimbi vya kisiasa kama vile mara kuwapandishia wenzao bei ya kusafirisha mafuta yao. S.Sudan sasa inasaidiwa na Israel ktk vita dhidi ya Sidan huku RWANDA NA UGANDA nao wakitishia kujiunga. ndugu zetu KHARTOOM walijaribu kujiunga na EAC wamekataliwa..jamani tuweni macho na mitego hii!!
Well said ndugu yangu
ReplyDeleteUkiondoa tatizo la jazba lililojitokeza kwa vijana wa Uamsho nadhani they are doing a fantastic work for the sake of Zanzibaris.
Hawa (Uamsho) hawana shida ya Uongozi au kuitawala nchi kama mifano ya nchi ulizozitaja shida yao ni kujaribu kusaidia na kuweka sawa pale ambapo Serikali inaonekana kukosea au kupotea njia.
Na tayari wana precedence waliposhiriki kikamilifu katika kuleta maridhiano na kuhamasisha waumini wa kiislamu hili limewasukuma na kuhisi kwamba kama waliweza kuangusha Muembe sasa watajaribu kuangusha Mbuyu.
Ninaamini kuna invisible hand inawasupport vijana hawa na kuna watchful eyes of the West monitoring them.
Ndugu yng wa mwanzo hapo juu umeongea ya msingi sn.ila nikwambie jambo moja.kwanza uamsho hawana shida ya uongozi wanataka haki ya znz.na km uliwah kuckiliza mikutano yao wanasema wanataka haki ya rais wao dk shein irud ktk hadhi yake.sio ss hv dk shein anaonekana km waziri asie na wizara.hebu funguka akili.umekaa kijinga jinga tu km huyu mwandishi wenu mapara.amabye hakupen habar kamili zinazohusu uamsho.mm nimeckiliza mihadhara yao yote na najua nn wanachokisema uamsho.taifa la znz linapotea.znz imeungana na nchi gan jamaniii?mbona hlo taifa la tanganyika halipo?na mbona tunaungana na taifa halina hata katiba.huhic kuwa ni njama ya kuipoteza znz?km hoja ni waznz wanganp wanaishi bara.mbona turkey na germany hazina muungano na kuna idadi ya waturuk milion 3 wanaishi ujeruman ije kuwa hao waznz elfu 40 walioko huko kwao.
ReplyDeleteInapendeza kusema kamba UWAMSHO hawana shida ya madaraka, lkn. uzoefu unaonesha vikundi vingi vya Kidini au kijamii baada ya kusaidia mabadiliko na kupata 'influence' ktk jamii, hugeuka vyama vya kisiasa ie; Muslim brother hood kule Misri na Twaliban Afghanistan.
ReplyDeletePili, kutokana na tofauti za kiimani kati yetu na MAGHARIBI mimi siamini kama kweli hiyo 'invisible hand' aliyoitaja mchangiaji wa pili inaweza kua na maslahi kwetu, sijui tu wazungu wanatutaftia balaa gani?
Waz'bari sote tunataka mabadiliko lkn. sio kwa JAZBA kama wanavyofanya UWAMSHO na wafuasi wao kama huyu mchangiaji wa pili.
Kwa mila zetu hapa huwezi kumwita mwenzako mjinga kwa kutofautiana mawazo.
Jengine nnaloliona ni kwamba watu wengi wanadhani tunaweza kuvunja MUUNGANO kwa jazba na chuki na bado mtu akawa na uhuru wa kuishi popote au kufanya biashara kati ya sehemu mbili hizi. Na ndio maana WATU wanatoa mifano ya Waturuki ml.3 wanaoishi Ujerumani au uhusiano wa kibiashara kati yetu na DUBAI lkn. hawatoi mfano wa NORTH NA S.KOREA hata kutembeleana hamna!
Watu wazima na akili na dini zetu, tunatoa maneno ya kibaguzi dhidi ya watu wengine wakati ni wazee wetu wenyewe walioiingiza Z'bar kwenye muungano na mkitaka kujua hayo hebu nendeni KACHORORA MASKANI( karibu na mchina tambi) mkasome lile bango ndio mtajua
Ili muungano uvunjike lazima tujue kiunagaubaga kwanini uliwekwa, kama tutashindwa kujua kwanini uliwekwa basi ni vigumu kuweza kuuvunja.
ReplyDeleteMchangiaji no 1 ni maneno unayosema ni ya kweli lakini ktk kutafuta haki lazma utakuta misukosuko mingi sana, na mara nyingi inachukua muda mrefu, kwa kesi ya Afghanistan waulize waengereza wao wenyewe taabani wanatafuta sabbu ya kurudi tu.Tafadhali usiangalie jambo kwa upande mmoja tu.
Waswahili husema, 'usitafunwe na uvi ukaonea tumba' na hili ndilo linalotokea Z'BAR kwa sasa!
ReplyDeleteMimi naamini mengi tunayoyalalamikia yamo ndani ya uwezo wa viongozi wetu kuyatatua isipokua tumeamua kuwaacha na kuandama wengine!
Lau kama juhudi wanayoifanya UWAMSHO leo hii, ingejikita ktk kukosoa uwozo yuliopo hapa, bila shaka Z'BAR ingeendelea mda mfupi tu ujao!
Kuwafanya watu waamini kwamba matatizo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yaliyopo Z'bar 'YOTE' yanatokana na MUUNGANO kwa kweli ni kuupotosha umma!
Binafsi, Mm ni miongoni mwa wale wanotaka mabadiliko makubwa( ktk mfumo wa muungano wetu) lkn. siungi mkono hoja ya kuvunjika.
WAHAFIDHINA lazima wanipe hoja makini, kwanini TUVUNJE na sio kurekebisha MUUNGANO?..Au wana lao jambo?
Najua watakimbilia hoja yao ya..oh huyu MAGENI lkn. mimi nawaambia Z'ar tukibaguana kwasababu ya tunatofautiana mitazamo basi hatobaki mtu , hata Amiri wetu (al-habib FARID) atarudi HADHRA-MUT YAMEN wakati Uislamu unakataza hayo!
Ndugu zangu sote lengo letu ni moja( kujenga Z'BAR bora na yenye ustawi wa watu wake) ila tunatofautiana plani ya ujenzi wenyewe.
Kwa hivyo wale wanaotukana tukana watu ovyo mtandaoni na kuwatafutia maeneo yao ya asili wajue wanabomoa!
Inaskitisha kuona hata huyu mwenye BLOG anaeturuhusu kutoa maoni yetu kwa uhuru na kubadilishana mawazo pia tunamtukana?.. kwanini na mimi nisifikirie kua wachangiaji wa namna hii nao z'bar ni wageni?..maana sisi hatuna silka hizi!
Mijadala ya iana hii haina tija "KUHOJI MUUNGANO NI SAWA NA MTOTO KUHOJI NDOA YA WAZAZI WAKE" la msingi ni kujadili the way foward.
ReplyDelete