Habari za Punde

LLOYD NCHUNGA AACHIA NGAZI YANGA

                                                  Llyod Nchunga  

Baada ya vuta ni kuvute iliyogubika Klabu ya Yanga baada ya kukumbwa na mikasa mingi ikiwemo kukumbwa na madeni na kufanya vibaya katika michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyomalizika mwezi uliopita, aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Llyod Nchunga ameachia ngazi.

Habari zilizotufikia muda si mrefu kutoka kwa wadau wa michezo zimesema Nchunga ametangaza uamuzi huo leo baada ya kinachoonekana maji kumfika shingoni.

Hatua hiyo, Nchunga ameichukua baada ya wiki iliyopita, Wanachama wa Klabu ya Yanga wakiongozwa na Kamati ya Mwafaka ya Wazee wa timu hiyo ya Jangwani  kukutana klabuni hapo na kutangaza kumfukuza.

Hata hivyo baada ya hatua ya wanachama hao ilipingwa na baadhi ya wadau wa michezo ikiwemo TFF kwamba hawakufuata taratibu za kisheria.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.