Na Masanja Mabula, PEMBA
MAHAKAMA ya wilaya ya Wete Pemba, jana iligeuka kuwa eneo la simanzi na majonzi kufuatia mshitakiwa wa kesi ya kuendesha gari bila ya hadhari na uangalifu kuanguka na kufariki dunia.
Mshitakiwa huyo marehemu Suleiman Said Abrahaman (40) wa Ziwani alifariki dunia muda mfupi baada ya kuanguka ghafla mahakamani hapo wakati akijianda kupanda kizimbani kusikiliza mashahidi dhidi ya shitaka linalomkabili.
Hakimu wa mahakama hiyo Nyange Makame Ali, alisema kabla ya kifo chake, marehemu huyo alikuwa na kesi ya kuendesha gari bila ya hadhari ambapo ni kinyume na kifungu cha 177(1) sheria za usafiri barabaraani No 7 /2003 ya Zanzibar.
Nyange alifahamisha kuwa mnamo Novemba 5 mwaka 2011 majira ya saa 11:00 jioni marehemu akiwa ni dereva wa gari ya abiria yenye No Z 489 AP akitokea Weni kuelekea Tungamaa aliligonga gari lenye No Z 290 CG mali ya Tahri nakulisababishia hasara ya shilingi milioni moja kwa makisio.
Kwa upande wake Daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo, Dk. Kurthum Abadhar Juma wa hospitali ya Wete, alisema kifo cha mshitakiwa huyo huenda kikawa kimesababishwa na mshituko ambao ulimkumba kabla ya kupanda kwenye kiriri.
Alisema kuwa mwili huo haukuwa na majereha yoyote na kwamba baada ya taratibu za kiuchunguzi, ulikabidhiwa kwa ndugu na jamaa kwa ajili ya mazishi.
Akizungumza na gazeti hili kamada wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Kamishna Msaidizi Mwandamizi Yahya Rashid Bugi, alisema marehemu huyo alipandishwa mahakamani hapo baada ya kushindwa kutimiza makubaliano ya kulipa gharama za matengezo ya gari alililoligonga.
Kamanda Bugi alisema kuwa awali marehemu huyo walikubaliana na mmiliki wa gari alililoligonga kulipana fidia kwa ajili ya matengenezo ya gari hiyo, lakini alishindwa kutimiza makubaliano na hivyo kujikuta akipelekwa mahakamani.
INNA LI LLAHI WA INNA ILAYHI RAJIUUN. ALLAHUMMA GHFIRLAHU WARHAMHU
ReplyDeleteSOTE NI WA ALLAH NA SOTE NI WENYE KURUDI KWAKE.
BINAANAM HAMNA KITU , TUKAE TUKIKUMBUKA MAUT, KWANI UKIAMKA ASUBUHI USIWE NA HAKIKA YA KUFIKA USIKU , NA UKILALA USIKU USIWE NA HAKIKA YA KUAMKA ASUBUKI. TUWE TAYARI WAKATI WOTE,NA TUJITAHID KUWA KATIKA MWAHALA NA MATENDO ANAYOTAKA ALLAH INSHAALLAH
some times makosa mengine wala si ya kutozana ma milioni, watu wana umasikini jamani munawatia presha tu
ReplyDeleteinna lillahi wa inna ilaihi rajiuun
inalilah waina ilaina rajuun....haya weye ulyemtoza mwenziwo mamilion ya pesa umeyapata sasa?jamani tusisahau ubinadamu eti kisa kuna sheria zetu hali ya kuwa tunazisahau za aliyetuumba...hzi ni salamu kwa uliyemtosa mwenzio mpaka kufikishana hapo
ReplyDeleteDuuu,...tena kweli.. hivoo!!!
ReplyDeleteinna lillah ainna ilaih raajuun. kwanini serikali haifikirii kuweka kwa kila mwenye gari BIMA ya lazima itengeze gari aliyo igonga? kama inavyofanywa katika nchi mbali mbali duniani!
ReplyDelete