Habari za Punde

Poulsen Ataja Kikosi Taifa Stars

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

SIKU chache baada ya kukabidhiwa mikoba ya kuifundisha timu ya soka ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’, Kocha Mkuu Kim Poulsen jana ametangaza kikosi cha wachezaji 25 wa timu hiyo,

Wanasoka hao wameitwa kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast, na wanatarajiwa kuingia kambini kesho.

Akitangaza kikosi hicho, Poulsen alisema esema uteuzi wake umezingatia uwezo wa mchezaji uwanjani, nafasi anayocheza na ubora wake.

Wachezaji walioitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius Munishi (Mtibwa Sugar).

Mabeki ni Aggrey Morris, Waziri Salum na Erasto Nyoni (Azam), Amir Maftah, Kelvin Yondani, Shomari Kapombe na Juma Nyoso (Simba).

Viungo ni Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude, Edward Christopher (U-20) (Simba), Salum Abubakar, Mrisho Ngasa (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), na Frank Domayo (JKT Ruvu- U20).

Washambuliaji ni Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe-DRC), Ramadhan Singano (Simba-U20), Simon Msuva (Moro United- U20), Haruna Moshi (Simba) na John Bocco (Azam).

Hata hivyo, kikosi hicho hakina sura yoyote kutoka wachezaji waliocheza ligi kuu ya Zanzibar msimu uliopita ambayo ilimalizika Mei 11, wala Wazanzibari wanaocheza soka nje akiwemo Ali Badru anayekipiga na Al Canal inayocheza ligi kuu ya Misri.

Stars iliyo chini ya udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro, imepangwa kucheza mechi ya kirafiki nyumbani Mei 26 mwaka huu dhidi ya Malawi kabla kuivaa Ivory Coast ugenini Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan.

5 comments:

  1. hii si taifa stars,bali ni tanganyika stars!
    Michezaji hiyo hiyo kila siku na hawana hata moja la maana wanalolifanya!

    ReplyDelete
  2. Haya Wazanzibar huo ndio Muungano hatutaki lawama.Maanake tuseme ndio mpira hakuna Zanzibar hata mmoja reserve tuwe hatuna ? Jamani tusiwe wajinga Wazanzibar, akufukuzae hakwambii toka.

    ReplyDelete
  3. Ama kweli mwenye chuki haoni!
    Yule Nassor Said (cholo) na Aggrey Morris ni wa wapi?

    Sisi kazi yetu lawama tu, na kutaka tuonewe huruma, badala ya kuwapigia kelele watu wetu wakaimarisha ligi yetu na kuacha longolongo au kuhamasisha vijana kwenda viwanjani tunabaki kulaumu.

    ReplyDelete
  4. Si wazenji peke yao, naskia hata yanga hawakutoa mchezaji hata mmoja!

    ReplyDelete
  5. HAWA UWAMSHO SIJUI HATA WANALOLITAKA, KWANI UKIACHA AGGREY MORRIS NA CHOLO YUMO PIA GOLIKIPA WA AZAM MWADINI ALI.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.