
IKIWA zimepita zaidi ya wiki mbili tangu kutwaa ubingwa wa soka Tanzania Bara, uongozi wa klabu ya Simba umemuongezea mkataba wa miaka miwili kocha wake Milovan Cirkovic.
Hatua hiyo imetokana na klabu hiyo kuridhishwa na kazi ya Mserbia huyo kwa kipindi cha nusu msimu tangu alipokabidhiwa mikoba ya kukinoa kikosi cha wekundu wa Msimbazi, kumrithi Mganda, Moses Basena.
Simba ilimaliza ligi na kutwaa ubingwa, ikiwafanyia mauaji makubwa watani wao wa jadi klabu ya Yanga kwa kuivuruga kwa magoli 5-0.
Makamu Mwenyekiti wa Simba Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, amefahamisha kuwa, Cirkovic ameongezewa mkataba na ataendelea na kibarua hicho kwa miaka miwili zaidi.
“Kipimo cha mafanikio ya kocha ni mataji na soka safi, kitu ambacho sisi kama viongozi tumekishuhudia chini ya Profesa Milovan, sasa hatuoni kwa nini tusimuongeze mkataba”, alifahamisha Kaburu.
No comments:
Post a Comment