Na Hamad Shapandu Pemba
WAKULIMA wa mpunga Kisiwani Pemba, wameelezea wasi wasi wao juu ya mavuno kidogo ya mpunga kama walivyojipangia , licha ya juhudi za serikali kuteremsha bei ya pembejeo.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, walisema matayarisho yao yaliaanza mapema, lakini juhudi za Wizara ya Kilimo zilionejana kusua sua, jambo ambalo linawapa hofu ya kufaidika na kilimo hicho.
Baraka Salim Ali mkaazi wa kijiji cha Mlindo Wingwi, alisema serikali iliyopo madarakani inastahili pongezi za aina yake kwa jinsi ilivyo jitayarisha mapema katika kupatia pembejeo wakulima licha ya mapungufu mengi yaliyojitokeza.
"Tunaipongeza Serikali kwa kuweza kutoa pembejeo na kujitayarisha mapema, lakini hadi sasa kuna mapungufu mengi yamejitokeza katika kilimo hichi", alisema.
Alifahamisha kuwa Mabwana Shamba, kwa kiasi kikubwa ni vikwazo na hivyo, kusababisha wakulima wengi kutofikia lengo kutokana na kukosa taaluma kwa wahusika.
"Wakulima wengi hawajui vipimo vya kutumia mbolea ya kusilia , mbolea baada ya kupalilia na matumizi ya dawa za kuulia magugu ni kikwazo kikubwa na iwapo hatua za dharura hazitochukuliwa, ikiwa hatutapelekewa watalamu wa kilimo ni wazi tunaweza kupoteza nguvu zetu bure". Alisema.
Mkulima huyo alisema katika ulimwengu wa leo wa sayansi na teknolojia ya kilimo ikiwemo kuachana na kijembe kongoroka na badala yake kutumia materekta , na pembejeo za kileo ni aibu katika msimu wa kilimo wizara husika kushinwda kufanya matayarisho ya uhakika na kusua sua kabla msimu hauja changanya.
Nae Makame Haji Makame , mkulima Tundauwa-Kilindo amelalamikia utaratibu wa ugawaji wa vituo vya kuuzia pembejeo , uhaba wa pembejeo zenyewe unakatisha tama pamoja na kutokuweko kwa materekta.
"Azma ya serikali yakuboresha kilimo bado ni mzaha wa maneno na uanzishaji wa majina katika orodha waliyonayo masheha ndio upate pembejeo limezidisha usumbufu hasa kama vile mbolea ya kusilia inayotolewa ni polo 10 tu huku akidai dawa ya magugu haipatikani kwa kutosha mkulima" alisema.
.
Nae Afisa Mdhamini wizara ya kilimo na mali asili Dk. Suleiman Omar alisema kuwa Wizara yake imejiandaa vyema bali utaratibu wa sasa uliopo wa daftari la wakulima haujazoeleka.
Amekiri mgao wa sasa wa mbolea ekari moja , mbegu ni kilo 25 , magugu , na mbolea inatolea hivyo hivyo ili kunusuru kuvunja kwa pembejeo hizo kutokana na ruzuku ya serikali ambapo pembejeo zote zinauzwa bei ya chini kabisa.
Amefahamisha kwa utaratibu huo una lengo la kuongeza udhibiti wa pembejeo kutosafirishwa nje ya nchi ambapo mfuko wa mbolea wa 15,000 Bara ni shilingi 60,000 na kuonya yeyote atakaekamatwa akikamatwa na utoroshaji wa pembejeo kukiona .
Amekiri upungufu wa mabwana shamba bali kwa upande wa pembejeo wanafungua vituo katika wilaya zote za Pemba kuondoa usumbufuhuo.
Hivi karibuni katibu mkuu wa Wizara ya kilimo Afan Othman Maalim alikiri mbele ya Rais wa Zanzibar katika Bonde la Ukele la Wilaya ya Micheweni- Mkoa wa Kaskazini Pemba kutokuweko kwa mapungufu ya mbegu na mbolea, kutokana na makisio kidogo ya mbolea ya awali, hata hivyo aliahidi kuongezwa kwa mbolea hiyo..
No comments:
Post a Comment