VIFAA vyenye thamani ya shilingi milioni nne vimekabidhiwa kwa wanavikundi vya mradi wa Ujasiria mali na Maisha, unaoendeshwa na TAMWA, kwa ufadhili kupitia shirika la UNIFEM, katika mkoa wa Kaskazini Pemba.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa Wanavikundi hao, ofisa uwezeshaji wa mradi huo Pemba, Jit-hada Abdalla Sali, aliwataka wanavikundi hao kuvitumia kwa ajili ya kujiletea maendeleo na kuondokana na umasikini.
Alisema kupatiwa vifaa hivyo ni moja ya harakati za TAMWA, kupitia mradi wake wa
WEZA katika kuhakikisha wanawake nchini wanajiendesha wenyewe na kuepukana na utegemezi.
Vifaa ambavyo mradi wa ujasiria mali na maisha, walivypatiwa ni pamoja na keni, mipira ya kumwagilia maji, charahani za kushonea, na za kufumia.
Jit-hada, alieleza kuwa kuwepo kwa vifaa majumbani kwa wanavikundi sio suluhisho la matatizo yao bali suluhisho ni kuvitumia kama inavyokusudiwa kwa nia ile ile ya mradi ya kujinasua na umaskini wa kipato.
Nao wanavikundi hao walitowa Shukrani zao kwa TAMWA, kupitia mradi huo kwa kuwapatia vifaa hivyo na kuahidi watavitumia ipasavyo kwani wao walishaonesha wanaweza pindipo wakiwezeshwa.
Vifaa hivyo vilitolewa katika maeneo ya Ole Kianga, Kangagani, Mjini Ole, Kiuyu, Kiungoni, Wingwi, Tumbe na Kisiwani kwa bit Abeid, katika mkoa wa Kaskazini Pemba , ambapo WEZA, ilikuwa ikifanyakazi na akinamama hao.
No comments:
Post a Comment