Habari za Punde

Zimbabwe kuijaribu Twiga Stars

DAR ES SALAAM

TIMU ya Taifa ya wanawake Tanzania katika mchezo wa soka, Twiga Stars, inatarajiwa kujipima ubavu na Zimbabwe katika mchezo wa kirafiki uliopangwa kufanyika Mei 12 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Twiga Stars hivi sasa iko katika ziara ya mechi za kirafiki katika mikoa ya Dodoma na Mwanza.

Katika ziara hiyo, jana ilitarajiwa kucheza na kombaini ya Mkoa wa Dodoma ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 kwenye uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma.


Katika mfululizo wa ziara zake za mazoezi, leo inaondoka Dodoma kwenda jijini Mwanza ambapo pia itacheza mechi moja ya kirafiki Mei 10 kwenye uwanja wa CCM Kirumba, na kurejea Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Zimbabwe.

Zimbabwe inatarajiwa kuwasili leo jioni kwa ndege ya South African Airways (SAA) ikiwa na msafara wa watu 25.

Kinadada hao wataondoka Mei 14 mwaka huu alfajiri siku moja baada ya mchezo wao dhidi ya Twiga Stars.











No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.