Amani nguzo ya
kukuza uchumi
Tume itumike
kuondosha kero ya Muungano
Na Ramadhan Makame
WAJUMBE wa Baraza la
Wawakilishi jana wamepitisha makadirio ya bajeti ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka
2012/2013, iliyowasilishwa wiki iliyopita na waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha
Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee.
Wajumbe hao
waliipitisha bajeti hiyo, baada ya kazi kubwa iliyofanywa na waziri huyo ya
kupokea michangio na kujibu hoja mbali mbali za wajumbe wa Baraza hilo .
Hata hivyo haikuwa
kazi rahisi kwani wakati Baraza hilo likikaa kama kamati ya kupitisha mafungu ya matumizi wajumbe hao
walilazimika kusimama mara kadhaa kupiga buti wakitaka ufafanuzi wa hoja
walizochangia.
Awali kabla ya
kupitishwa kwa bajeti hiyo wajumbe hao waliwaomba wananchi wa Zanzibar
kuhakikisha wanadumisha amani hali itakayohakikisha inastawisha uchumi wa Zanzibar .
Akichangia waziri wa
Biashara na Viwanda ambaye pia ni Mwakilishi wa jimbo la Mtoni (CUF), Nassor
Ahmed Mazrui, alisema kama Wazanzibari wataendelea kuichafua amali iliyopo
uchumi wa Zanzibar
utakuwa katika matatizo.
Alisema kwa kiasi
kikubwa uchumi wa Zanzibar unategemea utalii na
biashara, sekta ambazo haziwezi kuhimili vurugu na kwamba kama
yapo malalamiko dhidi ya Muungano yawasilishwe kwenye Tume ya mchakato wa
katiba mpya.
Naye Mwakilishi wa
jimbo la Magomeni (CCM), Salmin Awadh Salmin, alisema kama
Wazanzibari wanataka waendelee kupiga hatua mbele za kiuchumi lazima
wahakikishe amani iliyopo inadumu bila ya kuchezewa.
“Tunajua kama
matatizo ya Muungano yapo, na yapo kwa muda mrefu, tutumie fursa ya kusema
tunachokitaka na tusichokitaka”, alisema Mwakilishi huyo.
Kwa upande wake
Waziri Asiye na wizara Maalum, Haji Faki Shaali, alisema Tume ya katiba chini
ya Mwenyekiti wake Jaji Warioba, amesema atapokea maoni hata ya wale wasiotaka
Muungano.
“Kwa fursa hii
iliyopo watakaodhamiria kuvunja amani wana ajenda ya siri, kwanini wasitumie
nafasi hii kueleza yanayowasibu”,alisema waziri huyo.
Naye waziri wa Kazi
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika, Haroun Ali Suleiman, aliwataka
wananchi watumie fursa ya Tume kutoa maoni na asiwepo mtu wa kuzuiwa kutoa
maoni yake juu ya Muungano.
Katika michangio yao ya jumla wajumbe hao
waliishauri serikali kuhakikisha inatilia mkazo utekelezwaji wa Mapinduzi ya
kilimo, ambapo ni miongoni mwa sekta zilizopewa kipaumbele katika bajeti hiyo.
Mbarouk Wadi Mussa
(Mtando) –
Mipango mizuri
inabuniwa lakini tatizo lipo katika utekelezaji hali inayochangia wananchi
kushindwa kupata matunda ya mipango hiyo.
Serikali imepunguza
pembejeo za kilimo lakini wananchi wengi hawakunufaika nalo kutokana na mpango
wa kilimo utekelezaji wake kuwa mabaya.
Kwanini serikali
inapata kigugumizi kueleza utekelezaji wa mapendekeo ya kamati teule
imebainisha upotevu mkubwa wa fedha za umma.
“Serikali itueleze maana yale wananchi wanayajua sasa kwanini serikali inapata ugumu wa kueleza.
Mpango wa kukusanya
mapato bado uko lege lege, serikali haijawa tayari katika suala la ukusanyaji
wa kodi mianya ya kodi ipo mingi serikali ioneshe nia thabiti bado kunaudhaifu.
Sekta ya utalii bado
kodi zake hazijainufaisha sana
serikali wawekezaji wa kigeni wanapewa misamaha
Waziri aeleze
kwanini kodi ya wafanyakazi wa serikali ya Jamhuri walipo Zanzibar imeshindwa kukusanywa.
Serikali imefanya
jambo la maana kuweka kipaumbele sekta ya afya, akina mama wanaokwenda
kujifungua wasisumbuliwe.
Upo uuzwaji holela
wa majengo ya serikali, utaratibu uandaliwe uuzwaji wa majengo ya serikali
uhusishe baraza la wawakilishi japo kupitia kamati.
Bikame - ukuaji wa
uchumi unatia mashaka kwani hauoneshi kusaidia maisha ya wananchi.
Kipaumbele cha
kilimo serikali haikujipanga kumejitokeza changamoto kadhaa ikiwemo
kutopatikana kwa wakati pembejeo za kilimo. Mapinduzi ya kilimo yatafikiwa
endapo mipango itatekelezwa.
Serikali ijipange kama inataka kuhakikisha inatekeleza mapinduzi ya kilimo.
Udhibii wa Mfuko wa
bei uangaliwe unawaathiri wananchi kimaisha.
Rais apongezwa kwa
kuondoshwa ada ya akina mama wajawazito, maandalizi yaandaliwe ili mizwengwe
iondoshwe kwenye
Salmin Awadh Salmin
(Magomeni) –
Serikali inakusanya fedha katika taasisi zake kwa makadirio. Kodi
zisikusanywe kwa makadirio dunia imeondokana na njia hiyo ya ukusanyaji wa
kodi.
Utaratibu huo wa
makadirio ndio unaosababisha wa kudokolewa kwa mapato.
Kipaumbele cha
huduma ya afya,
Haji Faki Shaali - ada
ya bandari ya shilingi 1000 iliyoongezwa itatumika kunufaisha watoto wa
kizanzibari kwa kununuliwa madawati ya kukalia skuli.
Bajeti ya mwaka huu
ni nzuri kwani matumizi fungu la maendeleo ni kubwa kuliko fungu la matumizi ya
kawaida. Hali hiyo itaifanya nchi kupiga hatua.
Atakayefanya vurugu
atakuwa na ajenda ya siri kwani jaji Warioba amesema atapokea hadi maoni ya
wasiopenda muungano.
Wananchi waungane
kueleza yale yanayowakera katika kero za muungano.
Wazanzibari watafute
vitu vitakavyowaunganisha katika utoaji wa maoni ya katiba na kusahau tofauti
za kisiasa na kidini.
Nassor Ahmed Mazrui
Kukua kwa pato la
6.8 ni hatua kubwa utalii, biashara vimeimarika bidhaa kutoka Z’bar kwenda bara
2011 urari wa biashara kati ya T bara na Z’bar umekuwa 71.39 bilioni 74.73 urari 2010 tofauti ilikuwa zaidi ya bilioni
21
Karafuu nazo
zimesaidia seka ya bishara imekuwa mara tatu kutoka asilimia saba hadi 21,
mipango iliyopo ni kukuza aidi ya bishara
Utalii umekuwa mara
tatu zaidi
Serikali haikulala
juu ya suala la kuimarisha viwanda, kazi inafanyika kuhakikisha mazingira mazuri
yanawekwa kuvutia wawekezaji watakaoweka viwanda.
Suala la kukua kwa
biashara visiwani Zanzibar
linategemea amani na utulivu, amani ni nyenzo ya kujenga uchumi imara. Hakuna
mtu atakayekuja kujenga nchi hii.
Katiba tuitakayo
itapatikana kwa wananchi kujitokeza kutoa maoni umoja mshikamano kwa
Wazanzibari unahitajika katika muda huu kuliko muda wowote.
Kupita kwa bajeti nlikutarajia, wawakilishi wenyewe alina Omar Ali Shehe?..unatarajia nini hapo?
ReplyDeleteNi ajabu na kweli pale unapoona bajeti ikielekeza namna ya kujikwamua kutonana na utegemezi lakini wawakilishi wetu ndiyo vinara wa kukatisha jitihada hizo za kuondokana na utegemezi. Tozo ya kdi ya bandari kwa abiria kwenda Pemba ilikuwa sahihi kabisa kwa hivle wananchi watachangia upatikanaji wa madawati kwa ajili ya watoto wao kutoka kwenye nguvu za wananchi wenyewe. Lakini sasa itabidi madawati hayo yasinunuliwe na watoto waendelee kukaa chini wakati wawakilishi wakinesa kwenye viti barazani huku wakipata upepo mwanana wa air conditioners...
ReplyDeleteW'bari walimuelewa vibaya MZEE KARUME, pale alipoamua baadhi ya huduma za jamii ziwe bure, kwa vile ilikua ndio kwanza tunapata uhuru na hivyo wananchi walikua hawajajipanga.
ReplyDeleteLeo hii miaka takriban 50 tokea tupate uhuru lkn watu bado kila kitu wanataka kiwe bure, inapendeza lkn uwezo uko wapi?
Kweli Wazeji ni masikini lkn mambo mengine hayahitaji utajiri ni suala la kipaombele tu, hivi inakuaje mtu anaelalamikia umaskini lkn ana wake watatu au wanne?
Wakati umefika kwa SMZ kuacha kuongoza nchi kwa hisia, kama huduma inahitaji kuchangiwa serikali itoze mchango mara moja!
Mimi naamini kama SMZ itakua makini ktk kuchangisha baadhi ya huduma Wanachi nao watakua makini ktk kupanga familia. Hivi inakuaje mtu awena wake 4 na watoto 12 ategemee serikali kumsomeshea na kumtibia bure yeye anachangia nini serikalini? Aidha huduma za matibabu maalum kama vile KANSA, FIGO,INI, MOYO nk. serikali inatakiwa kutoa huduma hizi kwa malipo ili waweze kumudu kiziendesha na hivyo kuwapunguzia watu gharama zaidi za kwenda kutafuta huduma hizi idia, afrika kusini na Bara.
Najua wadau hawata nielewa lakini huu ndio ukweli Dunia nzima inafanya hivyo hatuwezi kua tofauti!...sasahivi karibia huduma zote za serikali zina suasua!
Ukitaka kuipata pepo lazima ufe...na tukitaka kupata madawati maskulini ni lazima tuchangie. Uhaba wa vifaa vya kufundishia na hata tiba vinatokana na wananchi kutochangia na kuwekwa vipaumbele. Tumepoteza nafasi muhimu sana ya kujikwamua kutokana na utegemezi wa misaada.
ReplyDeleteSioni sababu kwa wawakilishi kuwa katika kampeni zisizokwisha.