Habari za Punde

Ziara ya Mbunge Kutembelea Miradi ya Maendeleo ya Jimbo jilo

Jengo la Makau Makuu ya Wavuvi  Muembemadema, ambalo moja ya sehemu yake itatowa huduma ya kutowa mafunzo kwa Vijana wa Jimbo la Kikwajuni kwa Kazi za Amali na Mafunzo ya Komputer. mradi unaosimamiwa na Mbunge wa Jimbo hilo baada  kukamilika ujenzi wake unaofanywa na Mbunge.
Mbunge Mhe. Hamad Masauni, akizungumza na Wananchi na Vijana wa Jimbo la Kikwajuni alipotembelea miradi ya jimbo hilo, akiwa katika jengo la Wauvi muembemadema ambalo linafanyiwa ukarabati na kufunguwa kituo cha Mafunzo ya Kazi za Amali na Mafunzo ya Komputer, kwa Vijana wa Jimbo hilo.
Sheha wa Miembeni na  Mwenyekiti wa Kamati ya Uvuvi. Haji Shomari, akizungumza wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni alipofika kutembelea maendeleo ya ukarabati wa jengo hilo kwa ajili ya vijana.
Mwenyekiti wa Uvuvi Wilaya ya Mjini Salum Abdalla Mzee (Chepe) akitowa shukrani kwa mbunge baada ya kufanikisha ukarabati wa jengo hilo na kutowa kipaumbele kwa Vijana, ili kujipatia mafunzo ya Amali katika kituo hicho baada ya kumalizika ujenzi wake.
Jengo la Komputer kwa Wanafunzi wa Skuli ya Kiswandui, ikiwa ni mmoja wa Mradi wa maendeleo wa Jimbo hilo unaosimamiwa na Mbunge, ukiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake na kutowa huduma ya mafunzo ya Elimu hiyo.
Mbunge wa Kikwajuni akizungumza na Kamati ya Skuli ya Kiswandui, alipotembelea miradi wa maendeleo wa jimbo hilo ulioko katika skuli hiyo,ili kutowa elimu ya komputer kwa wanafunzi wa skuli hiyo. ikiwa ni moja ya masomo yao ili kupata uweleo na kufaulu vizuri elimu ya juu.
Mwalim Mkuu wa Skuli ya Kisuwandui Taifa Khamis Ahmeid, akitowa shukrani kwa Mbunge wakati wa ziara yake kutembelea mradi wa Chumba cha Komputer kwa mafunzo ya Wanafunzi wa Skuli hiyo, ili kuinua kiwango cha elimu na kizindisha ufaulu wa Wanafunzi katika elimu ya juu..  
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Yussuf Masauni, akizungumza na Viongozi wa SACCO Benki ya jimbo la Kikwajuni, alipowatembelea katika jengo hilo ambalo linafanyiwa ukarabati ili kufunguliwa benki hiyo kutowa mikopo kwa Wanavikundi wa Kikwajuni.
Mwenyekiti wa SACCOS Benki Bi.Tatu Tawakal, akitowa maelezo ya mradi huo wa Benki ya Saccos, kwa Mbunge alipofika kutembelea  mradi huo unaoendeshwa na Wanavikundi vya Jimbo la Kikwajuni. 

4 comments:

  1. Kaka umenikumbusha mbali, nimemwona mwalimu wangu wa primary Jang'ombe 1986, Bi Taifa, mwenye dira na mtandio mwekundu aliyefunga mikono(picha ya sita toka juu)

    Nadhani na hilo jengo la juu ni pale madema..ah..wakhti mapita!

    ReplyDelete
  2. Hongera Mbunge kwa kazi nzuri ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo letu - ilonikosha hasa ni ile kipande cha barabara kutoka kwqa Kamanda pale, ama hakika umaefanya jambo moja kubwa la busara.Mungu akujjaalie kila la kheri na mafanikio.

    ReplyDelete
  3. Mungu akuzidishie imani, mapenzi na ujasiri ndugu Masauni katika kuwatumikia wananchi wa jimbo la Kikwajuni na Zanzibar kwa ujumla.Malipo yako yapo kwa Allah Subhana wataalah..........!
    Mdau wa Calgary
    Canada

    ReplyDelete
  4. Tungepata wabunge watatu tu! kama huyu Hamadi Masauni basi Zanzibar na Tanzania kwa ujumla ingefika mbali sana kama itakumbukwa huyu kijana amekumbwa na misuko suko mingi sana kwa kuwatumikia wananchi lakini hakuvunjika moyo,tizama anavyolihangaikia jimbo lake wana wa Kikwajuni hatukumbuki Mbunge yeyote aliyejitahidi kama Masauni Mungu azidi kumpa uwezo wa kuwasaidia wananchi wa Kikwajuni na Zanzibar kwa ujumla,Hongera Hamadi Masauni.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.