Habari za Punde

CWT Yaitisha Mgomo wa Walimu Nchi Nzima

Na Mustafa Leu, ARUSHA
BARAZA la mkoa wa Arusha la Chama cha Walimu (CWT), limewataka walimu wote nchini kushiriki kwenye mgomo wa nchi utakaoanza Julai 7 mwaka huu, ikiwa ni shinikizo la madai ya nyongeza ya mishahara na posho za kujikimu na kufanya kazi kwenye mazingira magumu, na kuwata wazazi kuwaunga mkono katika mgomo huo.

Taarifa iliyotolewa jana mara baada ya kikao cha siku moja cha kujadili hatua za kuchukua kilichofanyika katika ofisi ya Chama cha Walimu, CWT, mkoa wa Arusha, imesema kuwa baraza limeridhia kuwepo kwa mgomo huo na kuwataka walimu wote kushiriki ikiwa ni shinikizo la kuitaka serikali kuwatimizia madai yao.

Taarifa hiyo imesama kuwa Walimu wanadai nyongeza ya mshahara ya 100%, posho ya kufanya kazi kwenye mazingira magumu, 55% na 30% ni posho ya kujikimu, nyongeza ambayo itawezesha walimu kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Baraza limesema kuwa kutokana na madai yao kutokushughulikiwa na serikali kwa kipindi kirefu sasa limeamua kuchukua hatua ya kutangaza mgogoro na serikali hatua ambayo itafuatiwa na mgomo wa walimu nchini ambao utafanyika mara baada ya walimu kujaza fomu na kupiga kura za kuunga mgomo Julai 7 mwaka huu.

Baraza limesema kuwa limefuata taratibu zote za kisheria na kuwatoa hofu walimu k,kuwa hakuna mwalimu atakae fukuzwa kazi kwa kushiriki mgomo huo kudai maslahi yao na limejipanga kuhakikisha hakuna mwalimu atakaechukuliwa hatua zozote za kinidhamu katika kutetea haki yake ya msingi.

Baraza limesema linaunga mkono maazimio ya Baraza kuu la taifa la CWT, lililofanyika mkoani Dodoma Juni 5 mwaka huu ambapo liliwataka viongozi waCWT, ngazi zote kutekeleza matakwa ya ya kutangazwa mgogoro kwa mjibu wa sheria za Ajira na mahusiano kazini,ya mwaka 2004 ,na baraza liliidhinisha kuwepo kwa mgomo ikiwa serikali itasindwa kutekeleza matakwa ya walimu ya kutaka kuongezewa mshahara kwa 100%. katika mgomo huo.

Baraza likatoa wito kwa wazazi nchini kukaa na watoto wao majumbani ili kuepuka kuwapatia usumbufu wakati wa mgomo wa walimu kwa sababu wakati wa mgomo huo walimu hawatafundisha .

Baraza limesewma kuwamgogoro huo ni wa kimasilahi ,kwa kuwa serikali haijawa tayari kukaa na Chama cha walimu nchini kutafuta ufumbuzi wa madai yao wana haki ya kutumia mgomo kama njia ya kutekelezwa madai yao.

Baraza kuu la taifa, limesema kuwa CWT, ilijaza fomu namba 1, ya kutangaza mgogoro na iliwasilishwa kwenye tume ya Usuluhi na Uamzi, Juni 8, mwaka 2012, na mgogoro huo haujatatuliwa hadi leo licha sheria kutaka mgogoro utatuliwe ndani ya siku 30.

Baraza limesema kuwa Wanaolalamikiwa kwenye mgogoro huo ni Mkuu wa Utumishi wa Umma, ambae ni Katibu mkuu kiongozi, Waziri wa Nchiofisi ya rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Katibu mkuu wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi,na mwanasheria mkuu wa serikali.

Baraza limesema kuwa fedha zipo na zimeshatolewa ila zinaliwa na wachache hivyo wanaishinikiza serikali ili walipwe na limewataka viongozi wa serikali kutokuwatishia walimu kwa kudai masilahi yao.

Baraza limeongeza kuwa walimu ndio wafanyakazi wanaodaiwa mikopo mingi kutoka katika taasisi mbalimbali za Umma na binafsi na hivyo wanaishi katika mazingira magumu ,wanalazimika kuingia kwenye mikopo kutokana na kulipwa maslahi duni wakati kazi wanzofanya ni kubwa mmno.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.