Habari za Punde

Dk Bilal Aiwakilisha Tanzania Mkutano wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Mazingira Endelevu Brazil


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa rais wa Zanzibar, Fatma Fereji, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, wakiwa katika Ukumbi wa mkutano, wakati walipohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Viwanja vya Ukumbi wa Mikutano, wakati alipofika kuiwakilisha nchi katikaMkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992. Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Francis Malambugi

Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa rais wa Zanzibar, Fatma Fereji, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa. wakiwa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.