Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa amri ya
kusitisha mgomo wa Madaktari
Kufuatia Tangazo la Chama cha Madaktari
nchini (MAT) la kuanza mgomo siku ya Jumamosi tarehe 23 Juni, 2012, Mahakama
Kuu ya Tanzania,Kitengo cha kazi,Dar es Salaam imetoa amri ya kusitisha mgomo
huo mpaka hapo pande zote mbili yaani Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania
(MAT) yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
·
Amri hiyo ya Mahakama imetolewa kufuatia maombi namba 73 ya
2012 yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa Serikali
dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).Sababu za msingi amabazo
zimepelekea Mahakama kuu kutoa amri hiyo upande mmoja ni pamoja na;
·
Iwapo mgomo huo utatokea utakuwa na kuwa amri hii isipotolewa
madhara yake ni makubwa isiyoweza kufidiwa kwa namna yoyote ile kama vile
kupoteza maisha n.k
·
Wajibu maombi,ambao ni
MAT, inaundwa na Madaktari ambao wapo katika Sekta ambayo inatoa huduma mahsusi
(essential service sector), Aidha Chama cha Madaktari Tanzania kimetangaza
mgomo bila kufuatia taratibu zilizoanishwa katika Kifungu cha 76(1 na 2) cha
Sheria ya Kazi (Employment and Labour Relations Act No 6 ya 2004.
Masharti hayo ni
·
Kuzuia wafanyakazi walio katika Sekta Muhimu kugoma na kama
wakigoma,
·
Kuwepona makubalianao ya pamoja ya kutoa huduma za msingi
wakati mgomo ukiendelea.
Kwa misingi hii,Mahakama Kuu ya
Tanzania, kwa Chama cha Madktari Nchini na wanachama wake kusitisha na
kutoshiriki katika mgonmo huo.
Jambo la maana sana!
ReplyDeleteHawa madaktari wanapewa kiburi na Chadema,mgomo uliopita ulichukua maisha ya jamaa yetu mmoja, aliondoka Z'bar kwenda Mulimbili akakutana na mgomo ikawa ndio mwisho wake.