Habari za Punde

Makamu wa Rais Dk. Bilal Afunga Maonesho ya Kwanza Tanzania ya Homes Expro

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akisiliza maelezo kuhusu matumizi ya Nyaya za Africab kutoka kwa Ofisa Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo, Khuzema Janowalla, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya kwanza ya Tanzania Homes Expro, yaliyofanyika leo Juni 10 katika Viwanja vya Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akisiliza maelezo ya ujenzi wa Nyumba 220 zinazojengwa eneo la Jangwani Beach, jijini Dar es Salaam, zinazotarajia kutumia jumla ya Sh. Milioni 208, kutoka kwa Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya Global Land Solutions Ltd, Murtaza Adamjee, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya kwanza ya Tanzania Homes Expro, yaliyofanyika leo Juni 10 katika Viwanja vya Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu utengenezaji wa Vigae vya ujenzi wa Nyumba kutoka kwa Ofisa Masoko wa Kampuni ya Insignia Ltd, Obed Machoka, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya kwanza ya Tanzania Homes Expro, yaliyofanyika leo Juni 10 katika Viwanja vya Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu ujenzi wa Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa, NHC, kutoka kwa Ofisa Masoko wa Shirika hilo, Mariam Ndabagenda, wakati Dk. Bilal  akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya kwanza ya Tanzania Homes Expro, yaliyofanyika leo Juni 10 katika Viwanja vya Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mauzo wa Shirika hilo, William Genya (wa pili kulia) ni Ofisa Mauzo mwandamizi wa Shirika hilo, Emmanuel Lymo.(Picha zote na Muhidini Sufiani. OMR)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.