Naibu Katibu Mkuu akiongea na waandishi wakati wa kufunga training program
Mhe. Masauni na Dr. Mshinda wakibadilishana machache wakati wa semina ya DTBi
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, ambae pia ni Mbunge wa Bunge la Africa na Mwanzilishi wa Taasisi ya Tanzania Youth Icon (TAYI), Eng. Hamad Yussuf Masauni akizungumza na waandishi wa habari na kuwashukuru Commission of Science and Technology (COSTECH). . Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa COSTECH, Dr. Hassan Mshinda, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dr. Patric Makungu, Mkurugenzi Mtendaji wa DTBI, Eng. George Mulamula na wa mwisho ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya DTBI Bw. T. Mlaki.
Eng. Masauni na Mshiriki kutoka Finland wakibadilishana mawasiliano
Washiriki wa Semina wakiwa katika picha ya pamoja.
Mheshimiwa Masauni aliwashukuru Dar Teknohama Business Incubator (DTBI) kwa kuipa dhamana TAYI (Taasisi ya Tanzania Youth Icon) ambayo Makao Makuu yake yapo katika Jimbo la Kikwajuni Zanzibar kuwa wenyeji wa Mafunzo ya Matumizi ya Teknolojia ya programu kwa kutumia Simu za Mikononi.
Mafunzo hayo kwa awamu ya pili yanyotarajiwa kuanza mwezi August 2012 yatadhaminiwa na DTBi, Nokia na Zantel
Mheshimiwa Masauni na Mwakilishi Mahmud Mohd Mussa juhudi zenu zinaonekana kwa jimbo lenu la Kikwajuni, jitahidini zaidi katika kuijenga Zanzibar mpya.
ReplyDeleteHichi kichwa hiki (Masauni) bado SMZ hawajakitumia ipasavyo!
ReplyDeleteNaamini tusingekua hapa tulipo!
Watu kama JUSSA, MASSAUNI, SADIFA, SAADA MKUYA, JOSEPH JOHN KILANGI na wengine wanaweza kabisa kuitoa Z'bar hapa ilipo! hawa vijana wanauwezo mkubwa!
huyu anayeongea na masauni mzungu ni kutoka marekani anaitwa joshua stern na si kutoka huko ulikosema...finland
ReplyDelete