Gari la Ng'ombe ndiyo usafiri mkuu wa wakaazi wanaoishi katika msitu wa hifadhi Masingini ambapo mdau alishuhudia jinsi usafiri huu ulivyo maarufu na unavyotumiwa sana na wakaazi wanaoishi maeneo hayo.
Hali ya msitu wenyewe kidogo inatisha kwani wananchi wanakata saana msitu. Sehemu nyingi zimeathirika na zimekatwa. Eneo hili ndio lenye kianzio kikubwa cha maji kwa ajili ya mji mzima wa Zanzibar na vitongoji vyake. ...tusipoziba ufa utajenga ukuta
Mkuu hili ni jambo la kuzingatiwa sana kuhusu uharibifu wa mazingira, tutilie neno huko kwa wanaohusika kuhusu umuhimu wa kuhifadhi misitu yetu, na serikali kuzidi kutafuta njia mbadala za wananchi kuwapunguzia kutokata misitu kwa ajili ya ujenzi, kuni na makaa.
ReplyDeleteKama kuna jambo linaloniumisha kichwa ni uharibifu wa mzingira!
ReplyDeleteJuzi, nilitoa maoni ktk makala ya mazingira ya mh. Fatma Fereji, kuna mtu akanambia hali ya utunzaji wa mzingira Z'bar umeimarika na akawa na shaka shaka kama kweli mimi nipo Z'bar
Sasa kweli huu ndio utunzaji wa mzingira kweli? miti mikubuwa inakatwa ovyo halafu eti tunahangaika kupanda mipya!
Hii ni sawa na kujenga ktk maeneo yenye rutba kama vile MWERA, FUONI nk halafu tukanunua maeneo ya uwanda tukapanda miti eti tuna KHUISHA!
Nimejaribu sana kutafuta Mwakilishi ili nimpe maoni yangu kuhusu hazingira kabla ya kikao lkn. kila mmoja hapatikani anaona ataomba pesa!