MADA: MCHANGO WA
HISTORIA NA UTAMADUNI KATIKA KUKUZA
SEKTA YA UTALII ZANZIBAR
DKT. AMINA A. ISSA,
IDARA YA MAKUMBUSHO NA
MAMBO YA KALE
MAANA NA AINA ZA UTAMADUNI
Mji Mkongwe karne ya 19 |
Utamaduni
ni mfumo kamili wa maisha wenye kujumuisha mila, silka, desturi za jamii
Utamaduni
na wa aina 2
Utamaduni
unaoshikika (tangible), majengo ya kale, vitabu, zana za kazi, ala za muziki
Utamaduni
usioshikika (intangiable), lugha, hadithi, muziki, ngoma
MAANA YA HISTORIA NA
MAENEO YA KIHISTORIA
Historia
ni matukio ya kale
Historia
ni lazima ihusishwe na watu ambao ndio wanaopelekea kuwepo vitu, matukio
Inaweza ikawa ni historia ya nchi, jamii, watu, eneo,
majengo, kijiji au hata historia ya kuanza kwa teknolojia, maendeleo ya
kisayansi n.k.
Maeneo ya kihistoria (historical sites) ni zile zenye
umuhimu mkubwa kwa jamii.
Maeneo hayo huhifadhi historia, utamaduni na maendeleo
ya nchi kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Maeneo ya kihistoria ni kama maeneo ya wazi
(landscape) miamba, visiwa (islands), caves (mapango), makaburi (tombs).
Mifano ya maeneo ya wazi ya kihistoria: Kaliwa-Tumbe,
Bandari Kuu, Unguja Ukuu na Mtambwe Mkuu
Majengo ya kihistoria: majengo ya kale (monuments),
makumbusho (museums), magofu (ruins)
Eneo la kihistoria pia hujumuisha eneo la ardhi
iliyoungana na sehemu ya karibu ya eneo hilo (buffer zone)
UHIFADHI WA MAENEO YA
KIHISTORIA
Uhifadhi
ulianza 1923 – Idara ilipoundwa
Makumbusho
zilianzishwa 1925 na 1930
Sheria
ilianza 1927
1941,
Hamam la Kidichi likaanza kuhifadhiwa
Sheria
ya sasa ni ya 2002: inahusu usimamizi,
utunzaji, hifadhi, kuyatangaza na kuyafanyia matengenezo
Ni
urithi wa utamaduni
Kuyaweka
majengo katika hali yake ya ukale
Kuzuia
uharibifu
Kuhifadhi
historia yetu
Ni
chanzo cha kujipatia elimu
Mifano:
Msikiti wa Kizimkazi, Ngome Kongwe, Mji Mkongwe, Beit-el Ajaib, Msikiti wa Ba
Mnara
Idara ina hifadhi maeneo na majengo 83 kama ifuatavyo:
Mahodhi au Mahamam
Makasri
Nyumba za Ibada: Misikiti, Makanisa na Mahekalu
Ngome
Chemba za watumwa
Maeneo ya miji ya kale
Viwanda
Makaburi
Majengo ya kale
Visiwa
Mapango
KWANINI UTALII ZANZIBAR?
Jengo la Makumbusho |
Zao
la karafuu pekee halikutosheleza
Kupanda kwa bei ya petroli, 1973
Vita vya Tanzania na Uganda, 1979 – 1981
Kuanguka kwa kambi ya Usoshalisti
HATUA
sera za mabadiliko ya kiuchumi (Economic
Liberalization Policy)
mikakati ya ubinafsishaji (privatization)
Serikali ni mmiliki pekee wa njia kuu za uzalishaji
mali (State Ownership)
MCHANGO WA HISTORIA KATIKA
UTALII
Kielelezo halisi cha kujua utamaduni wetu
Nyenzo ambayo wataalamu na wasomi huitumia katika
kuandika historia ya nchi
Maeneo ya kihistoria huchangia katika kukuza uchumi wa
nchi
Kutambulika kwa historia ya Zanzibar ulimwenguni
‘UTALII KWA WOTE’ NA MAENEO YA KIHISTORIA ZANZIBAR
Maeneo ya Kihistoria Zanzibar |
Maeneo ya kihistoria ni amana yetu sote
Wananchi wahamasishwe kuyatembelea maeneo hayo ili nao
waweze kushajiisha jamii
‘Sera ya Urithi wa Utamaduni’ ni muhimu izingatie
kuwahusisha wananchi katika kuyaendeleza maeneo ya kale
Wanajamii wapewe mafunzo juu ya kukuza na kuuendeleza
utalii na kuyatunza maeneo ya kihistoria
Mipango ya kuhuisha na kuuendeleza utalii izingatie
aina na shughuli za utalii kulingana na mazingira yao
‘Utalii kwa wote’uwe pia ni chachu ya kukuza utamaduni
wa jamii au nchi
Wananchi wawe ni wadau wakuu wa mambo ya utalii
Maeneo ya kihistoria yawe ni sehemu ya mchanganyiko wa
shughuli za kiutamaduni
Kuanzishwa kwa makumbusho za kijamii zitasaidia
kuwakilisha historia, mila na silka za Zanzibar
HITIMISHO
Maeneo ya kihistoria ili yawe ni chanzo cha maendeleo
ya nchi inabidi yahifadhiwe na iwe ndiyo dira ya Taifa
Bila ya kuhifadhiwa maeneo hayo, Zanzibar itapoteza
historia na utamaduni wake.
Kaka ahsante kwa kuzingatia maoni ya wadau kwa kutuletea sio tu picha za kihistoria bali pia elimu ya historia na utamaduni.
ReplyDeleteKaka kwa kweli sisi wenye kupenda kujua mambo tunafaidika sana na Blog hii.
Allah, akupe nguvu na uwezo wa kufanikisha hilo!
Hata hivyo inaonekana kuna matatizo kidogo ktk hii makala kwani haisomeki viziro
Hii program ilikuwa katika power Point sasa wakati qwa kuibadilisha kuja kwenye word format ndipo hayo madudu ndipo yalipotokea tustahamiliane
ReplyDeleteNimependa sn maana na mimi mnazi wa utamaduni.
ReplyDelete