Na Ameir Khalid
MABINGWA wa Afrika Masharikiti na Kati timu ya soka ya Yanga inatarajiwa kufugua dimba dhidi ya timu ya Jamhuri, katika mashindano yaliopewa jina la Tanzania Cup.
Pambano hilo la ufunguzi litapigwa Julai mosi saa 10:00 jioni katika uwanja wa Amaan.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) timu nane zitachuana kwenye ngarambe hizo, ambazo zimegawiwa katika makundi mawili ya A na B.
Kwa upande wa kundi A litakuwa na timu za Yanga, Zanzibar All Stars, Jamhuri na Super Falcon, wakati kundi B linazijumuisha timu za Simba, Azam, Mafunzo na timu ya taifa ya vijana U – 23.
Kiingilio katika pambano hilo itakuwa shilingi 10,000 VIP, shilingi 5000 na shilingi 4000 kwa jukwaa la urusi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Afisa Habari wa ZFA, Munir Zakaria, usiku kutakuwa na mtanange mwengine kati ya Zanzibar All Stars dhidi ya mabingwa wapya wa Zanzibar, Super Falcon.
Mechi ya tatu itapigwa Jumatatu ya Julai 2 wakati wawakilishi wa Zanzibar katika mashindano ya Kagame klabu ya Mafunzo itacheza dhidi ya mabingwa wa Vodacom Tanzania Bara, Simba mechi ambayo itachezwa saa 10.
Usiku timu ya taifa ya vijana U-23 itatiana mikononi na mabingwa wa Mapinduzi Cup klabu ya Azam.
Jumanne Super Falcon itashuka tena kuwakabili kaka zao Jamhuri, wakati usiku Yanga itacheza na Zanzibar All Stars. 
UTHAMINI WA FIDIA MRADI WA SGR KIPANDE CHA SITA TABORA-KIGOMA WAENDELEA KWA 
KASI
                      -
                    
Na Munir Shemweta, WANMM 
Zoezi la uthamini maeneo yatakayopitiwa na ujenzi wa Mradi wa Reli ya 
Kisasa SGR kipande cha 6 kutoka Tabora hadi Kigoma linaen...
12 hours ago

No comments:
Post a Comment