Habari za Punde

Zanzibar Yaendelea Kuboronga Copa Cocacola

Na Ameir Khalid
UKITOA timu ya Mkoa wa Mjini Magharibi ambayo inafanya vyema, timu nyengine za Mkoa ya Kaskazini Unguja na Kusini Pemba zinazoshiriki michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Copa Cocacola, zimeendelea kuboronga katika michunao hiyo baada ya hapo juzi kupokea vipigo, kutoka kwa timu walizokutana nazo.

Akizungumza na gaezeti hili kwa njia ya siu kutoka Dar es Salam katibu wa chama cha soka (ZFA) Wilaya ya Mjini, Yahya Juma Ali mara baada ya kumalizika kwa mapambano hayo.

Alisema timu ya Mkoa wa Kaskazini Unguja ilikubali kupokea kipogo cha magoli 2 – 1 kutoka kwa timu ya Mkoa wa Mara, mchezo ambao ulivurumishwa uwanja wa Tamko Kibaha Mkoa wa Pwani.

Nao vijana wa Mkoa wa Kusini Pemba wamekubali kipingo cha magoli 4 –1 kutoka kwa vijana na Mkoa wa Arusha, mtanange ambao ulivurumishwa katika dimba lenye nyasi bandia Karume Ilala jijini Dar es Salam.

Wakati vijana hao wa RC Tindwa wakipokea kipigo hicho ndugu zao wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, imeendeleza wimbi lake la kutoka sare baada ya kufungana goli 1 – 1 dhidi ya Mkoa wa Manyara na kumaliza mechi zake hatua ya makundi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.