Na Mwanajuma Abdi
IKIWA leo dunia inaadhimisha siku ya dawa za kulevya, imelezwa tatizo hilo bado ni kubwa ambalo linahitaji nguvu za pamoja katika kupambana nalo.
Mkurugenzi Idara ya Kupambana na Udhibiti wa Dawa za Kulevya kutoka Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Ahmed Awadh Salim aliyasema hayo jana, wakati akifungua mkutano wa siku moja wa maadhimisho ya siku ya dawa ya kulevya uliondaliwa ZAYEDESA.
Alisema tatizo la dawa ya kulevya badoni kubwa, ambapo katika nchi za Ulaya hutumia hadi silaha katika kupambana nalo.
Aidha alieleza kwa Zanzibar imeweza kupambana na dawa za kulevya baada ya vijana kukubali kubadilika, hasa ikizingatiwa kuwa wao ndio waathirika wakubwa na ndio nguvu kazi ya taifa.
Alisema jumuiya mbali mbali ikiwemo ZAYEDESA na nyumba za kurekebisha tabia ‘Soba House', zimeweza kupunguza tatizo hilo ilinganishwa na miaka 15 iliyopita.
Awadh aliipongeza jumuiya ya ZAYEDESA kwa kuinga mkono juhudi za Serikali kupita Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais kwa kupiga vita jangwa hilo.
Alisema leo mataifa mbali mbali duniani yataungana katika kuadhimisha siku hiyo, ambapo nchini yalianziwa kwa usafi wa mazingira.
Nae ofisa Mipango wa ZAYEDESA, Umukurthum Ansell alisema jumuiya hiyo imekuwa ikiendeleza mapambana na madawa ya kulevya ili kuokoa nguvu kazi ya taifa ambao wengi wao watumiaji wake ni vijana.
Nao washiriki wa mkutano huo, wateja waliopata nafuu, ambao walisaidia kwa njia moja ama nyengine na ZAYEDESA walisema walipokuwa wakitumia madawa hayo walikosa samani kwa familia zao na kuonekana wanyama kama paka na mbwa wanasaminika kuliko wao.
Akitoa ushuhuda wake Ramadhan Said (Pawawindo) alisema wakati alipokuwa akitumia madawa hayo alijihusisha na wizi wa pawawindo za gari, ambapo kwa sasa ameamua kuachana kabisa na tabia hiyo, sambamba na kuishukuru jumuiya hiyo kwa kumuwezesha kufika hapo alipo kwa sasa.
Akifunga mkutano huo, Mratibu wa mradi wa ZAYEDESA, Mgoli Lucian Mgoli, alisema wanaendelea kutao taaluma kwa vijana kuacha pamoja na vita juu ya maambukuzi ya Ukimwi.
Alifahamisha kuwa, wanapata faraja kuona vijana wanaamua kubadilika tabia kuacha matumizi ya madawa ya kulevya, kwa vile baadhi yao wanapata maambukizi ya ukimwi kutokana na kuchangiana sindano na vitu vyengine vyenye ncha kali pamoja na kujihusisha na ngono zisizo salama.

No comments:
Post a Comment