Habari za Punde

Meya Ataka Walimu Walipwe kwa Wakati

Na Fatuma Kitima, DAR ES SALAAM

SERIKALI imetakiwa kutilia mkazo mishahara ya walimu kuwalipa kwa wakati kwa kuwa walimu ni watu muhimu nchini.

Akitoa taarifa hiyo wiki iliyopita katika hafla fupi ya kumuaga Mwalimu mkuu wa shule ya Mwongozo pamoja na kutoa pongezi kwa mwalimu aliyestaafu.

Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songolo Mnyonge alisema kuwa tatizo hilo ni kubwa, hivyo linawaathiri sana watoto hasa katika kipindi cha migomo.

“Mimi nashindwa kuelewa hii serikali inafikiria nini kuhusu maslahi ya walimu ili kuepusha migogoro ya mara kwa mara inayotokea hapa nchini”, alisema Mnyonge.

Alisema kuwa hakuna mtu muhimu hapa nchni kama mwalimu kwa kuwa kila mtu lazima apelekwe skuli ili aweze kupata elimu ambapo asilimia 90% ya malezi ya watoto ni walimu na sio mzazi.

Alisema Mwalimu mkuu wa shule ya Mwongozo Elly Mshuma ni mfano wa kuigwa kwa kuwa ya Mwongozo ilipofika sasa sio ilipokuwepo awali.

Naye Mkuu wa skuli aliyekuwa akiagwa Elly Shuma alibainisha kuwa yeye alipoanza kufundisha skuli ya Mwongozo alikutana na changamoto nyingi hivyo alitumia muda mwingi kutafakali nini kifanyike ili kuboresha skuili hiyo.

Awali skuli ya Mwongozo ilikuwa haina madawati na baadhi ya watoto walikuwa wanakaa chini pindi wanapojifunza.

Kutokana na changamoto hiyo alijitahidi kufanya kila linalowezekana kuomba misaada kutoka sehemu mbalimbali ili kuweza kuboresha skuli hiyo na kuweka mazingira mazuri kwa wanafunzi.

Alitoa mwito kwa walimu wa skuli hiyo kuendelea na ushirikiano na kufanya kazi kwa pamoja na mwalimu mkuu aliyopo ili kuweza kuendeleza skuli hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.