Na Mwanajuma Mmanga
HALMASHAURI ya wilaya ya Magharibi imekadiria kukusanya fedha jumla ya shilingi milioni 480.7 kupitia vianzio vyake mbali mbali vya mapato kwa wilaya magharibi Unguja.
Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2011 hadi 2012 kwa halmashauri hiyo ilikadiria kukusanya jumla ya shilingi milioni 400 ambapo bajeti hiyo ilivuka makadirio na mafanikio ya kukusanya shilingi milioni 3007 zimetumika katika miradi ya maendeleo, na shilingi milioni 321 kwa kazi za ofisi.
Katibu wa Halmashauri hiyo, Bakari Khatib Shaaban, alieleza hayo wakati alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wake huko ofisini kwake Mombasa juu ya suala zima la uwajibikaji wa kazi zao ili kuona malengo ya bajeti mpya imefanikiwa kwa kiasi fulani.
Nae ofisa tawala wa wilaya ya Magharibi, Mohammed Ali aliitaka halmashauri ya wilaya ya Magharibi ibadilike katika ukusanyaji wa mapato katika kudhibiti vyema vianzio walivyonavyo katika ukusanyaji wa mapato katika kuibua vianzio vipya.
Sambamba na hayo, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Diwani wa Wadi ya Mbuzini Masoud Abrahman Masoud alisema kwa mwaka wa fedha 2011-2012 umeweza kutekeleza malengo yote waliyojiwekea kutokana na kuomba malengo ya Bajeti waliitarajia.
Alisema mafanikio hayo yalitokana na ushirikiano mkubwa waliokuwa nao maafisa wa Halmashauri, madiwani na watendaji wengine katika shughuli mbali mbali za kazi.
Hata hivyo, alisema bado Halmashauri imekuwa na changamoto kwa baadhi ya wafanyabiashara na wananchi kutolipa ada zinazotozwa kutokana na leseni za Biashara, ada za taka, ujenzi na mauziano.
No comments:
Post a Comment