Mh. Waziri wa Habari, Utamaduni,Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk, amefanya uteuzi na amemteua Nd. Suleiman Mbarouk Suleiman kuwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya sensa na Filamu za Maonyesho. Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa kifungu No.13 (1) ya Sheria ya Bodi ya Sensa na Filamu za Maonyesho.
Aidha amemteua Nd. Kassim Haji Salum kuwa Katibu Mtendaji wa ZFA Taifa. Uteuzi huo umefanyika kama Katiba ya ZFA Kifungu No.41 na 42 inavyoeleza.
Uteuzi huo unaanza tarehe 18 Juni, 2012.
Kwa hatua zako.
NB. Kabla ya uteuzi wa Nd. Kassim, nafasi ya katibu Mtendaji ilikuwa ikihudumiwa na Nd. Mzee Zam Ali, aliestaafu kazi kisheria.
Abdi Sh. Abdullah
OFISA MAWASILIANO - WHUUM
No comments:
Post a Comment