Habari za Punde

Dk Shein Afutarisha Pemba


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kushoto) akijumuika na Viongozi na wananchi wa Mkoa wa kaskazini Pemba katika chakula cha Futari aliyowaandalia katika viwanja vya Ikulu ya Wete pemba jana.{Pichana Ramadhan Othman,Ikulu.}

Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba,wakiwa katika chakula cha Futari waliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Ikulu ya Wete Pemba jana. {Pichana Ramadhan Othman,Ikulu.}




Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba,Dadi Faki Dadi,akitoa shukurani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein,kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wake baada ya chakula cha Futari alkiyowaandalia katika viwanja vya Ikulu ya Wete pemba jana. {Pichana Ramadhan Othman,Ikulu.}


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) pamoja na wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba,wakiitikia dua iliyoombwa na Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi,baada ya chakula cha Futari,huko Ikulu ya WEte Pemba jana. {Pichana Ramadhan Othman,Ikulu.}

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akiagana na Viongozi na wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba jana baada ya Chakula cha Futari aliyowaandalia katika viwanja vya Ikulu ya Wete Pemba. {Pichana Ramadhan Othman,Ikulu.}
Baadhi ya akina mama wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiitikia Dua iliyoombwa baada ya chakula cha Futari katika Mwezi mtukufu wa Ramadhan,iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,Ikulu ya Wete pemba jana. {Pichana Ramadhan Othman,Ikulu.}

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein,(katikati) akiitikia dua na viongozi akinamamawa Mkoa wa Kaskazini Pemba baada ya Chakula cha Futari iliyoandaliwa kwa wananchi ho huko Ikulu ya Wete Pemba jana. {Pichana Ramadhan Othman,Ikulu.}

Na Rajab Mkasaba, Ikulu


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein jana aliungana na wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika futari maalum aliyowaandalia wananchi hao. 

 Hafla hiyo ilifanyika huko katika viwanja vya Ikulu ndogo ya Wete na kuhudhuriwa na wananchi hao pamoja na viongozi mbali mbali wa dini, Serikali na vyama vya siasa.

 Miongoni mwa viongozi hao ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe. Dadi Faki Dadi, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Mwinyihaji Makame, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih. 


 Akitoa neno la shukurani kwa mahudhurio yao makubwa wananchi hao kwa niaba ya Alhaj Dk. Shein, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba alieleza kuwa Dk. Shein amefarajika kwa ushiriki wa wananchi hao katika futari hiyo maalum aliyowaandalia. 

 Nao wananchi hao walieleza kufarajika kwao na muwaliko huo wa Rais na kueleza kuwa hatua yake hiyo inaonesha wazi mapenzi, busara, hekima na jinsi anavyowajali wananchi wake pamoja na maamrisho ya MwenyeziMungu na Mtume wake Mohammad S.A.W. 

 Wananachi hao walimuombea dua kwa MwenyeziMungu na kumuombea aendelee kongoza nchi kwa salama, amani, utulivu na uvumilivu mkubwa sanjari na kuendelea kuongoza nchi kwa kupata maendeleo makubwa. 

 Wakati huo huo pia. Mama Mwanamwema Shein nae alishiriki katika futari hiyo akiungana na akina mama wenzake kutoka sehemu mbali mbali katika Mkoa huo pamoja na viongozi wa dini, serikali na vyama vya siasa na wananci kwa ujumla. 

 Leo Alhaj Dk. Shein anatarajiwa kufutari pamoja na wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba huko katika viwanja vya Ikulu ndogo Chake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.