Na Shaib kifaya
31-7-2012
Alisema lengo kuu
la ukusanyaji wa maoni hayo kwa wananchi hao ni
kutoa maamuzi ya kuchagua mfumo upi wa katiba wanaoutaka wananchi hao
ili kuweza kutumika hapa nchini
aliyasema hayo huko mkoani wakati alipo kuwa katika zoezi hilo likiendelea.
Warioba alisema
kila mwananchi anayo haki ya kuto maoni yake nasio kufuata maoni ya mtu mmoja
mmoja kwani kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake kwa uoni wake na kile anacho
kipenda yeye mwenyewe kukichagua .
Aidha alisema
maoni hayo yanayo tolewa na wananchi hao yatafikishwa kwenye tume hiyo na kuya chambua kwa
kuyafanyia kazi kwani alisema kila mwananchi ambae amechangia utoaji wa
maoni juu ya katiba ambayo anaitaka yatafanyiwa kazi.
Warioba
alifahamisha kwamba baada ya kwisha kuchambua maoni hayo ya tawasilishwa kwenye
Bunge la katiba kwa kutoa uwamuzi wakile kilicho jadiliwa juu ya maoni hao.
Naye mjumbe wa
Tume hiyo Docter Mvungi,ambaye pia ni mwanasheria alisema katiba ndio kitu
muhimu katika nchi ili iweze kutoa huduma kwa misingi ya haki na usawa .
Alisema kwamba
wananchi ndio wenye katiba ambayo katiba hiyo itapatikana baada ya kumalizika
utowaji wa maoni hayo kwa wananchi wote wa Tanzania .
Hivyo aliwafahamisha wananchi hao kuwa katika
Tume hiyo kuna Bunge la Katiba ambalo linaongozwa na Baraza la Wawakilishi Zanzibar ,Bunge la Jamuhuri ya mungano wa Tanzania pamoja na vyama vya Siasa na asasi za
kiraia ambapo hapo mwanzo Bunge hilo
halikuwepo
No comments:
Post a Comment