Na Shaib Kifaya 31-7-2012
MKUU WA wilaya ya Mkoani, Jabu khamis Mbwana
amewataka wananchi wa Chambani Makombeni kuwapa ushirikiano mzuri makarani wa Sensa
watakapo pita katika maeneo wtakayo pangiwa kufanya kazi hiyo ya kuhesabu watu
.
Alisema zoezi hlio
la Sensa ambalo lina tarajiwa kufanyika tarehe 26-8-2012 kwa lengo la kupata
idadi kamili ya wananchi hao ili Serikali iweze kupanga mipango yake kwa
maendeleo ya nchi wake aliyasema hayo nyakati tofauti wakati alipo kuwa akiwa
hutubia wananchi hao kuhusu sensa.
Jabu alifahamisha
kwamba kila inapo fika miaka kumi ni lazima ifanyike Sensa kwani ndio kitu
muhimu sana kwa
Serikali kwani inapata takwimu halisi na kujua matatizo yaliomo katika nchi .
Sambamba nahayo
aliwataka wananchi hao kwamba kuna baadhi ya watu wa dindi wanapita mitaani
wakiwa hamasisha wananchi kuto kukubali kuhesabiwa kwani nijambo ambalo
linamnyima mwananchi kufanya wa jibu wake
Jabu aliwanasihi
wanachi kuto kubali kushawishiwa na watu wa aina hiyo kuto kuto maoni kwani ni
kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi hao kwani kuna weza kukosa taarifa muhimu
katika kaya .
Pia aliwatoa hofu
wananchi hao kwamba maelezo yote yatakayo tolewa wakati wa sensa yatabakia kuwa
nisiri na karani wa sensa na mweye kaya ambaye ndie mtoa taarifa.
Nae Afisa Tawala
wa Wilaya hiyo, Abdalla saluma Abdalla aliwataka akina mama kwani wao ndio watu
wanao bakkia majumbani kuhakikisha kwamba wakati watakapo pita makarani wa
sensa wanawapatia taarifa kwa ufasaha bila ya kuwa woga .
Aidha alifahamisha
kwamba ilesiku ya sensa mtu ambaye amelala pale siku ile ya mkesha wa kuamkia
sensa ndie atakae hesabiwa katika eneo lake alilolala
kwa siku ile .
No comments:
Post a Comment