Khadija Omar Juma, ZJMMC-PEMBA.
Zaid ya Bilioni mbili zimetolewa na taasisi inayojishuhulisha nautoaji wa mikopo kwa
wafanya biashara wadogo wadogo na wakati na kati kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo
Hashim Kassim Zaid huko ofisini kwake Chake Chake
Pemba alipokuwa akizungumza na
wandishi wahabari.
Amesema kuwa,
kati ya fedha hizo walizozitoa kwa ajili ya mikopo ni kuanzia shilingi
laki mbili hadi kufikia milioni mbili wakati
aina ya mikopo hiyo meki na fahari.
Aidha
alifahamisha kuwa,mikopo yafahari huanzia shilingi laki 3 hadi kufikia milioni
25. Wakati huo huo mkopo wa meki hutolewa kuanzia sh laki mbili hadi kufikia
milioni mbili.
Kuhusu
changamoto zinazo wakabili katika
taasisi hiyo amesema kuwa wanachama wa pride hawana usafiri wauhakika na
wanachama hawalipi inavotakikana kutokana
hali ya pemba ilivo ngumu jambo ambalo linarudisha nyuma harakati zao.
Pride Pemba ilianza 2004 na jumla ya wanachama wake ni 223
meki ni 173 na fahari ni 50.
No comments:
Post a Comment