Habari za Punde

Fainal ya Kombe la ZAWEDA Jimbo la Kitope Unguja.

Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza, akimkabidhi Kombe la Ubingwa na ZAWEDA , nahodha  wa timu ya Newstar ya Kiwengwa Masoud  Maulid, baada ya kuishinda timu ya White Kids ya Mahonda,katikati Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama  Mbunge wa Kitope Bi.Asha Seif Balozi. mchezo uliofanyika uwanja wa Kitope. 1--0 
Mwakilishi  wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza, akimkabidhi  Seti ya Jezi na Mpira Nahodha wa timu ya  White Kids, Ussi Ali, baada timu yake kuibuka mshindi wa Pili wa michuano hiyo. 
Mwakilishi wa jimbo la Uzini Mhe.Mohammed Raza na Mke wa Mbunge wa jimbo la Kitope Mama Asha Balozi.wakibadilishana mawazo wakati wa  mapumziko ya mchezo huo wakiwa na wajumbe  wa kamati ya michuano hiyo.
Mhe Raza akikagua timu ya White Kids ya Mahonda

Mhe Raza akikagua timu ya Newstar ya Kiwengwa.

Beki wa timu ya White Kids kulia Tahir Kassim, akijaribu kumzuiya mshambuliaji wa timu ya Newstar Issa Haji.katika mchezo wa fainal uliofanyika uwanja wa Kitope.l

Mshambuliaji wa timu ya White Kids, akiwatoka mabeki wa timu ya Newstar
Wapenzi wa mpira wa miguu katika Jimbo la Kitope  wakifuatilia mchezo wa fainali ya Kombe la ZAWEDA zilizofanyika uwanja wa kitope.
Wapenzi wa mpira wa miguu katika Jimbo la Kitope wakifuatilia mchezo wa fainali ya Kombe la ZAWEDA zilizofanyika uwanja wa kitope.
Vijana wakizirudi ngoma za kizazi kipya wakati wa fainali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.