Habari za Punde

Sauti za Busara 2013: Wito wa filamu za muziki wa kiafrika

Tamasha  la Sauti za Busara linapokea maombi ya filamu za muziki wa kiafrika kwa ratiba  ya mwaka 2013.

Toleo la kumi  la tukio  hili muhimu litachukua nafasi yake kuanzia tarehe 14-17 Februari ndani ya  ukumbi wenye historia ndefu wa Ngome Kongwe,  Zanzibar.

 Sauti a Busara inatafuta filamu tofauti kutoka pande zote za Afrika ambazo  zitawaburudisha na wavutia wenyeji na wageni. Zinaweza kuwa video za muziki,  rekodi za matamasha, makala za muziki au filamu za kiuchunguzi. Filamu bora  zitachaguliwa na kuonyeshwa katika skrini kubwa kabisa  kipindi cha tamasha.

Filamu inayoelezea muziki au mwanamuziki  kutoka bara la Afrika na kwingineko.
Filamu inayoelezea hazina na utofauti  wa muziki wa Afrika masahriki na kwingineko.
Filamu za muziki zitakazowavutia  watazamaji wageni na wenyeji.
Filamu yenye muonekano mzuri, ubora wa  sauti na vilevile muziki uliotoka Afrika.
Filamu mpya na sauti zisizowahi  kusikika, na wasanii wapya
Filamu za kigeni ni lazima ziwe na tafsiri  ya kiingereza au kiswahili

Fomu za maombi na taarifa zaidi zinapatikana katika  tovuti ya Sauti za Busara, busaramusic.org Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 16 Novemba 2012.
 

Tamasha  la Sauti za Busara ni tukio la kila mwaka ndani ya Afrika Mashariki na ambalo  linajulikana kama “Tamasha rafiki ndani ya sayari”.

Toleo lijalo la mwezi wa  pili 2013 litakutanisha wanamuziki 200: vikundi zaidi ya ishirini kutoka Afrika  Mashariki na kwingineko, na wote hao hufanya maonyesho yao moja kwa moja kwa  asilimia mia(100% live)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.