Meneja Masoko wa Kampuni ya Unga wa Ngano ya AZANIA Tanzania Mohammed Bashrahil, akionesha moja ya Jezi aliokabidhi timu ya Baraza la Wawakilishi .
Naibu Spiuka wa Baraza la Wawakilishi Ali Abdalla , akikabidhiwa mipira na Meneja Masoko wa Kampuni ya AZANIA Mohammed Bashrahil, kampuni hiyo imekabidhi vifaa vya michezo jezi seti na mipira kwa ajili ya timu hiyo, katikati Mwenyekiti wa Timu hiyo Hamza Hassan, makabidhiano hayo yamefanyika katika jengo la Baraza Chukwani.Zanzibar.
Msaidizi Meneja wa timu ya Waheshimiwa Wawakilishi Nassor Salam Jazeera, akitowa shukrani kwa Kampuni ya AZANIA kwa msaada wao kwa timu yao ili kuweza kushiriki vizuri katika michuano inayoshiriki timu hiyo katika michezo ya kirafiki inayofanya timu yake ndani na nje ya Zanzibar.
Meneja Masoko wa Azania Mohamed Bashrahil akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi vifaa kwa timu ya Waheshimiwa wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
No comments:
Post a Comment