Habari za Punde

Mzee Yussuf kupamba kampeni CCM

Na Mwantanga Ame
 
BENDI ya muziki wa taarab Jahazi Modern, inatarajiwa kupamba uzinduzi wa kampeni za mgombea wa uwakilishi wa jimbo la Bububu (CCM) Hussein Ibrahim Makungu (Bhaa), zitakazofunguliwa leo.
 
Kundi hilo litakuwa chini ya kiongozi wake Mzee Yussuf.
 
Bhaa alimtangaza msanii Mzee Yussuf na kundi lake kuwa ndiye atakayenogesha uzinduyzi huo, alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM, tawi la Bububu Wilaya ya Magharibi Unguja juzi.
 
“Msanii Mzee Yussuf na kundi lake la Jahazi, amejitolea kuzipamba sherehe za uzinduzi wa  kampeni zetu kuelekea uchaguzi mdogo, kwa kutoa burudani ya muziki mzito”, alisema mgombea huyo.
 
Aliwataka wanachama wa CCM, kujitokweza kwa wingi kumuunga mkono, ili kwa pamoja wafanikishe kampeni na hatimaye kulitia mikononi  jimbo hilo.
 
Kampeni hizo za CCM zinatarajiwa kuanza kesho Jumapili, ambapo mbali na chama hicho, uchaguzi huo pia unashirikisha vyama vyengine tisa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.