Mwandishi wa Habari wa Chanal Ten Muniri Zakaria akiuluza maswali katika Kikao kilichofanywa na Wawakilishi wa CCM kutoa kauli ya Kulaani machafuko yanayoendelea ambayo yamesababisha kuchomwa Moto Maskani ya CCM ya Kisonge Mjini Zanzibar
Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Hamza Hassan CCM akifafanua jambo katika Kikao kilichofanywa na Wawakilishi wa CCM kutoa kauli ya Kulaani machafuko yanayoendelea ambayo yamesababisha kuchomwa Moto Maskani ya CCM ya Kisonge Mjini Zanzibar.
PICHA NA-MAKAME MSHENGA -MAELEZO ZANZIBAR
Wajumbe
wa baraza la wawakilishi (ccm) wamelaani vikali vitendo vinavyoendelea kufanywa
na jumuiya ya mwamsho kwa kuvunja amani, utulivu na kusababisha vurugu katika
mji wa zanzibar kuanzia jana.
Hapo jana
kundi la mwamsho lilivamia nyumba za watu maduka na kupora bidhaa kadhaa katika
maduka na kusababisha hasara kubwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari huko mbweni kwenye ukumbi wa baraza la wawakilishi, mhe.
Hamza Hassan Juma kwaniaba ya wawakilishi wa Ccm amesema wakati umefika kwa
serikali kuchukuwa hatua zinazofaa kabla hali haijawa mbaya zaidi.kwani
kuendelea kukaa kimya kwa Serikali kutatoa sura mbaya kwa wananchi.
Amesema
serikali imeunda serikali ya umoja wa kitaifa ili kuondoa kasoro zilizokuwepo
na kuwafanya wananchi kuishi kwa amani na usalama na kuweza kuondoa tofauti zao
za kisiasa.
Amesema
isifike pahala Zanzibar ikawa kama zile nchi zenye machafuko na kuwafanya
wanachi wake kushindwa kuishi kwa amani na salama.
Hivyo
wajumbe hao waliitaka serikali mara moja kuwachukulia hatua wale wote ambao
wamehusika na ghasia hizo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Aidha
wamemtaka mkuu wa Jeshi la Polisi IGP na makamanda wenzake kuwajibika moja kwa moja
juu ya suala hili ili kukomesha mambo hayo.
Halkadhalika
wajumbe hao waliitaka serikali kulipa fidia mali zote zilizoharibiwa kutokana
na fujo hizo na kuviruhusu vikosi vya
smz vkusaidia katika kuweka ulinzi na usalama ili maafa zaidi yasije yakatokea.
Akizungumzia
suala la kufutwa jumuiya hiyo, Mhe. Hamza amesema jumuiya ya mwamsho si chama
cha siasa ni jumuiya ya kidini lakini imeonekana kukosa muelekeo na kufanya
vitendo vinavyowafarakanisha waumini wa dini hiyo, kuwagawa. na kuidhalilisha
dini yenyewe ya kiislam.
Hivyo
waliitaka taasisi inayohusika kuifuta Jumuiya hiyo kwa vile inakwenda kinyume
na malengo na dhamira ya kuanzishwa kwake.
Kuhusu
kutoweka kwa Sheikh Farid, Mhe. Hamza amesema hadi hivi sasa haijulikani wapi
alipo na nani aliyeyemchukuwa au kumteka nyara kwa vile kwa mara ya mwisho
inasemekana alikuwa na dereva wake.
Wajumbe
hao leo waligoma kuingia katika baraza wakilaani kitendo hicho na kusema kwamba
kesho watapeleka hoja binafsi kwa spika wa baraza hilo ili kujadiliwa suala
mwamsho na vitendo vyake dhidi ya serikali .
No comments:
Post a Comment