Habari za Punde

Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aongoza Watanzania katika maziko ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Mzee Cleopa David Msuya katika Kijiji cha Chomvu, Usangi Wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na waombolezaji mara baada ya Ibada ya mazishi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Mzee Cleopa David Msuya katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mwanga, Usharika wa Usangi kivindu, wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro tarehe13 Mei, 2025. 


Viongozi mbalimbali waliohudhuria mazishi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Mzee Cleopa David Msuya katika Kijiji cha Chomvu, Usangi Wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro tarehe13 Mei, 2025. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi wengine katika mazishi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Mzee Cleopa David Msuya nyumbani kwake katika Kijiji cha Chomvu, Usangi, wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro tarehe13 Mei, 2025. 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiweka udongo kwenye kaburi la  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Mzee Cleopa David Msuya katika maziko yaliyofanyika nyumbani kwake Chomvu, Usangi Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro tarehe13 Mei, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye kaburi la  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Mzee Cleopa David Msuya katika maziko yaliyofanyika nyumbani kwake Chomvu, Usangi Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro tarehe13 Mei, 2025. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.