Habari za Punde

Meli Nne Saccos Yaadhimisha Miaka 20

Naibu Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Juma Makungu  Juma akizungumza jambo na Katibu wa Melinne Saccos Bi Njuma Ali Juma wakati wa Sherehe ya  Maadhimisho ya miaka 20 ya Melinne Saccos na Mkutano Mkuu wa 15 huko katika ukumbi wa melinne  Saccos,

 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Juma Makungu Juma  akizindua Maadhimisho ya miaka 20 ya Melinne Saccos na Mkutano Mkuu wa 15 huko katika ukumbi wa melinne  Saccos.

Baadhi ya Wanachama wa Melinne Saccos  wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe.Juma Makungu Juma (hayupo pichani) wakati wa Sherehe ya  Maadhimisho ya miaka 20 ya Melinne Saccos na Mkutano Mkuu wa 15 huko katika ukumbi wa melinne  Saccos,
Baadhi ya Wanachama wa Melinne Saccos  wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe.Juma Makungu Juma (hayupo pichani) wakati wa Sherehe ya  Maadhimisho ya miaka 20 ya Melinne Saccos na Mkutano Mkuu wa 15 huko katika ukumbi wa melinne  Saccos.

Serikali itaendelea kutekeleza dhamira yake ya kuwanyanyua wananchi kiuchumi kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo vikundi vya ushirika ili kusaidia kukuza vipato vya wananchi na kuongeza ajira kwa vijana.

Akizungumza katika Maadhimisho ya miaka 20 ya Melinne Saccos na Mkutano Mkuu wa 15 kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe.  Dk. Sada Mkuya Salum, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe.Juma Makungu Juma amesema ili kufikia malengo hayo iko haja ya viongozi kutoa elimu ya kuhamasisha vikundi mbalimbali pamoja na wanachama jinsi ya kuweka akiba na mikopo kwa lengo la kuimarisha maendeleo yao pamoja na ushirika.

Aidha amewataka kudumisha Umoja na mshikamano katika uendeshaji wa ushirika huo  kwa kuepukana na  migogoro mifarakano ya wanachama isiyokuwa ya lazima .

 

Mhe.Makungu alitumia nafasi hivyo kuwataka kudumisha  Umoja huo Kwa dhamira ya kusaidiana ili kustawisha hali za wanachama kwa kukabiliana na hali za umasikini sambamba na kuendeleza suala la Amani upendo mshikamano kwa kuachama na Masuala ya ubaguzi ili kuendeleza kupata mafanikio zaidi.


Nae Katibu wa Melinne Saccos Bi Njuma Ali Juma amesema miongoni mwa Mipango mikakati ya ushirika huo ni kumaliza Jengo la ghorofa tatu pamoja na kupunguza asilimia ya mikopo kwa wanachama  ili kupata mafanikio zaidi .


 Aidha amesema kuwa Kamati ya mikopo imefanikiwa kutoa mikopo ya fedha Kwa wanachama 591, wakiwemo wanaume na wanawake pamoja na vikundi 17 vya ushirika  yenye thamani ya 2,287,500,000 pamoja na mikopo iliyorudishwa ni 1,884,358,700.sawa na asilimia 82 ya marejesho ya mikopo iliyotoka.


Akitoa wito Kwa wanachama hao amewataka kuengeza mashirikiano yao ili ushirika uzidi kuimarika sambamba na  kutumia pesa zao kwa malengo ili wanachama waweze kufanya marejesho kwa wakati.


Kwa Upande wa Mshika fedha wa Melinne Saccos Shemsa Saleh Hilali alisema mafanikio makubwa yamepatikana ikiwemo kuongezeka Kwa mtaji wa ushirika kutoka Shilingi 4,369,608,257 Kwa mwaka Hadi kufikia 4,919,168,637 Kwa mwaka 2024, zinazotokana na Akiba, Amana na Hisa.


Kwa Upande wa Mkaguzi wa vyama vya Ushirika Hasina Suleiman Rashid akitoa ripoti ya ukaguzi kwa mwaka 2024 ya Melinne Saccos .amesema ameridhishwa na ushirika huo ambao imeonyesha maendeleo na mafanikio makubwa bila ya kujitokeza ubadhirifu 

Mapema akisoma  risala ya Melinne Saccos Hafsa Juma Ussi amesema dhamira ya ushirika huo ni kusaidia kuibua kustawisha na kuimarisha hali za wanachama ili waweze kukidhi mahitaji Mbali mbali ya kiuchumi na kuondokana na umasikini wa kipato.

 

Amesema ushirika huo ilianza 2005 ikiwa na mtaji wa shilingi laki sita hadi sasa imefanikiwa kuengeza  mtaji hadi kufikia Shilingi Bilioni 4,919,168,637 kwa mwaka 2024 vilevile umefanikiwa kupokea wanachama wapya 245 ambao wamejiunga katika  Saccos hiyo  jambo ambalo litasaidia  kuimarisha ushirika huo

 Akitoa neno la shukrani Sheha wa Shehia  ya Melinne Nomal Maulid Salum amempongeza  Naibu Waziri huyo Kwa ujio wake wa kuunga mkono maadhimisho hayo jambo ambalo limeonyesha faraja kwa wanachama.


Amesema  Melinne Saccos  ni kiyoo Cha Zanzibar Kwa kuweza kuekeza Sukuk Kwa lengo la  kumuunga mkono Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  katika jitihada za kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.


Nao Wanachama wa Melinne Saccos wamesema kupitia Saccos hivyo wameweza kupata mafanikio mbali mbali ikiwemo ya kiuchumi na kimaendeleo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.