Rais Kikwete ni Mwenyekiti wa Tume ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo amepewa jukumu na viongozi wenzake ndani ya Jumuiya hiyo kukutana na viongozi wa Madagascar kuwaelezea maamuzi ya mkutano wa viongozi hao wa SADC uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dar Es Salaam.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, mwanzoni mwa wiki hii, Mheshimiwa Ravalomanana alithibitisha kuwa amekubaliana na maamuzi ya viongozi wa SADC.
Miongoni mwa mambo mengine, viongozi hao wa SADC wanataka viongozi hao wawili wa Madagascar washawishiwe na wakubali kutogombea katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika nchini humo mwakani
No comments:
Post a Comment