MWANDISHI WETU
Tarime
SERIKALI imewataka wafanyakazi wa sekta ya madini kuwa watulivu wakati inafanyia kazi malalamiko yao kuhusu fao la kujitoa katika mifuko ya hifadhi ya jamii, ambapo amesema inaandaa utaratibu maalumu utakaowawezesha wanachama wa mfuko husika kunufaika nao wakiwa kazini ama baada ya kumaliza utumishi wao.
Serikali imewasisitizia wafanyakazi nchini kuwa suala hilo limepewa kipaumbele ili kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.
Ari hiyo ilitolewa hivi karibuni na Waziri wa Ajira na Kazi, Gaudensia Kabaka, wakati akizungumza na wafanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG) wakati wa ziara yake kwenye mgodi huo uliopo wilaya ya Tarime, mkoa wa Mara.
Waziri huyo aliwasihi wafanyakazi wenye mawazo ya kuacha kazi ili tu wachukue
mafao yao ya kujitoa kuachana na fikra hizo potofu ambazo alisema zitaleta athari kwa familia zao.
Bi.Kabaka amesema serikali imesikia kilio cha wafanyakazi we sekta ya madini na wengine na kwamba kwa pamoja na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), wako katika jitihada za kuangalia jinsi ambavyo wanachama walioandikishwa kwenye pensheni kama wanaweza kuanzishiwa utaratibu wa kuweka na kukopa yaani "supplementary scheme."
"Serikali haijafikia uamuzi wakati wowote wa kufanya kuhusiana na mtu ama watu wanaotaka kujitoa katika fao hilo ndio maana niko hapa," alisema.
Alitangaza kuwa serikali itakutana na SSRA na watu wa sekta ya madini jijini Dar es Salaam tarehe 7 Januari, kwa ajili ya kupata mawazo yao juu ya suala la mafao ambapo wafanyakazi wa Migodini watawakilishwa na wawakilishi wao amabo ni chama cha wafanyakazi.
Alisema kuwa serikali haina haraka juu ya suala hilo kwa kuwa inataka kusikiliza mawazo ya wananchama wote, Watanzania, wabunge na wadau mbalimbali ili kupata maoni ambayo yatatafsiriwa kisheria.
Alisema serikali itawasikiliza Watanzania ili kujua ni nini wanapenda kiwepo katika masuala ya hifadhi ya jamii kwa sababu sheria na sera siyo msahafu hivyo inaweza kubadilika kila mara kutokana na mahitaji ya wakati husika.
Waziri Kabaka pia alitembelea miradi mbalimbali ya jamii inayofadhiliwa na mgodi huo wa Barrick na kuisifu kampuni hiyo kwa kusaidia jamii.
Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule mpya na ukarabati mkubwa wa kituo cha afya cha Nyangoto.
Duu! inaonekana kiswahili kwa wenzetu bado tatizo na sisi bado hatuko tayari kuwasadia kama wenye lugha.
ReplyDeleteKwa mfano; kichwa cha habari hapo juu kinasema FAO lkn. kiukweli hatuna FAO bali MAFAO.
Maneno kama vile maradhi, mapishi mafao n.k. wenzetu yanawasumbua na hudhani yapo ktk hali ya wingi na hivyo kuyalazimisha kuwa umoja.
Bara kuna mamneno ya kiswahili hata hao maprofesa wa kiswahili wanashindwa kujua namna yanavyotumika jambo ambalo linatia shaka ktk huo uprofesa wao.
Mfano;
1) mtu husema" nimekodisha nyumba" akimahanisha "nimekodi nyumba"
2)utaskia mtu "nifanyaje?" akimahanisha "nifanyeje?"
3)mtu anasema" mke wangu nimemshindwa" akikusudia" mke wangu amenishinda au mke wangu nimemshinda(haniwezi)
4)wengine husema" mimi na mke wangu, tumeshindwana"
Hii angalau inakubaliana na mnyambuliko wa kisarufi yetu!
Jamani tusipowasaidia hawa jamaa watatuharibia lugha...wao hawakuipenda hii bali MWALIMU Aliwalazimisha kwa hivyo wanafanya 'KANYAGA TWENDE' wakidhani wanamlaani MAREHEMU!