
Beki wa Coastal Union akiupitia mpira kwenye miguu ya mshambuliaji wa Azam, Seif Abdallah usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi. timu hizo zilitoka 0-0

Suleiman Kassim 'Selembe' akimuacha chini Khamis Mcha 'Vialli'

Hatari langoni mwa Coastal
Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
AZAM FC na Coastal Union ya Tanga zimetoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani hapa.
Coastal leo ndio waliotawala mchezo na kupoteza nafasi kama tatu za wazi za kufunga mabao, kutokana na umakini mdogo kila walipopata nafasi hizo.
Azam walipata nafasi moja nzuri kipindi cha pili, lakini walinzi wa Coastal walisimama imara na kuondosha kwenye hatari jaribio hilo.
Katika mchezo huo, kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Samir Hajji Nuhu, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Salum Abubakar, Humphrey Mieno, Gaudence Mwaikimba, Kipre Tchetche/Brian Umony dk 24 na Hamisi Mcha ‘Vialli’/Seif Abdallah dk 66.
Coastal Union; Juma Mpongo, Ismail Khamis, Othman Tamim, Philip Metusela, Mbwana Khamis‘Kibacha’, Hamisi Shengo, Suleiman Kassim ‘Selembe’/Hussein Twaha dk 50, Jerry Santo, Mohamed Mtindi, Soud Othman/Razack Khalfan dk90 na Danny Lyanga/Joseph Mahundi dk 90.
Katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo, Miembeni iliitandika mabao 4-1 Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa mao Dze Tung.
Mabao ya Miembeni yalitiwa kimiani Adeyum Saleh Ahmed dakika ya 41 na 72, Mohamed Hamdani na Rashid Roshwa dakiaka ya 74, wakati la Mtibwa la kufutia machozi lilifungwa na Juma Mpakala dakika ya 10.
No comments:
Post a Comment