Mshambuliaji wa timu ya Azam Brain Omony akimpita beki wa timu ya Tusker. Timu ya Azam imeshinda 2-1
Mfungaji wa timu ya Tusker akishangilia ushindi wa timu yake baada ya kufunga goli la kwanza.
Muamuzi wa mchezo wa Fainal kati ya Azam na Tusker Kibo ilibidi asimamishe mchezo huo kwa dakika tatu kumtoa nje Mwanadada huyu ambaye ameingia uwanjani kupitia jukwaa la urusi, inasemekina Mwanadada huyu ana matatizo ya akili.
Wachezaji wa timu ya Azam wakishangilia timu yao baada kufunga goli lapili, wakati ikicheza na timu ya Tusker katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa Amaan.
Mshambuliaji wa timu ya Azam Gaudence Mwaikimba akimpita beki wa timu ya Tusker. Timu ya Azam imeshinda 2-1
Wapenzi wa timu ya Azam wakishangilia timu yao, wakati ikicheza na timu ya Tusker katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzin uliofanyika uwanja wa Amaan.
Wachezaji pamoja na wapenzi wa timu ya Azam wakishangiria baada ya kuitoa Tusker ya Kenya
Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimkabidhi Kombe la Ushindi wa Pili Nahodha wa timu ya Tusker Joseph Shikokoti timu ya Tusker ya Kenya imeshika nafasi ya Pili ya Michuano hiyo ilofanyika katika uwanja wa Amaan.
Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Mapinduzi Cup, Nahodha wa timu ya Azam Hamid Mkami.baada ya kuifunga timu ya Tusker ya Kenya katika mchezo wa Fainal ya Kombe la Mapinduzi uliofanyika katika uwanja wa Amaan.
No comments:
Post a Comment