Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya bwawani kuhusiana na maoni yake juu ya mabadiliko ya katiba. Maoni hayo aliyasilisha rasmi jana mbele ya tume ya mabadiliko ya katiba iliyoongozwa na mwenyekiti wake jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba.Kushoto ni Waziri wa Habari Said Ali Mbarouk.
Waandishi wa habari wakifuatilia maoni ya Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika hoteli ya Bwawani Zanzibar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akionyesha warka wa maoni yake kuhusu mabadiliko ya katiba kwa waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika hoteli ya bwawani Zanzibar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akibadilishana mawazo na mwandishi mwandamizi wa shirika la AP nd. Ali Sultan, baada ya mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika hoteli ya Bwawani. (Picha na Salmin Said, OMKR)
No comments:
Post a Comment